Kocha wa zamani wa Taifa Stars Marcio Maximo akimpa Rais Jakaya Mrisho Kikwete zawadi ya jezi ya timu ya Democrata anayofundisha nchini Brazil alipokwenda kumsalimia Rais katika hoteli ya Tivoli jijini Sao Paulo.
Kocha wa zamani wa Taifa Stars Marcio Maximo akisalimiana na Rais Jakaya Mrisho Kikwete alipokwenda kumsalimia Rais katika hoteli ya Tivoli jijini Sao Paulo.
Kocha wa zamani wa Taifa Stars Marcio Maximo akimsalimu mke wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete alipokwenda kuwasalimia katika hoteli ya Tivoli jijini Sao Paulo.Picha na IKULU
Na Anna
Nkinda – Sao Paul, Brazil
18/04/2012
Vilabu vya soka nchini
vimeshauriwa kuwa na timu nzuri kuanzia ngazi ya watoto wenye umri wa miaka
nane, vijana na kuendelea ili kupata timu bora ya Taifa.
Wito huo umetolewa na
aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa Star Marcio Maximo wakati
akiongea na waandishi wa habari mjini Sao Paul.
Maximo alisema kuwa timu
nyingi ambazo ni bora na zinafanya vizuri katika mchezo wa soka zimekuwa
zikiwaandaa watoto wenye vipaji vya mchezo huo wangali wadogo ili waweze kuwa
wachezaji wazuri hapo baadaye.
Kocha Maximo pia alikutana na
kufanya mazungumzo na Rais Jakaya Mrisho kikwete, ambapo alimnshukuru sana Rais
kwa ushirikiano wa hali ya juu aliompa wakati alipokuwa akiifundisha Taifa
Stars miaka takriban mitatu iliyopita.
Kwa upande wake Rais Kikwete
alimpongeza Kocha Maximo kwa juhudi zake za kuendeleza soka la Tanzania,
akimwambia uwepo kwake Tanzania kuliasidia sana kuiweka nchi katika ramani ya
mchezo huo.
Rais Kikwete alikubaliana na
kocha huyo kwamba ili timu ya Taifa ifanye vyema ni lazima maandalizi yaanzie
ngazi za chini, ikiwemo vilabu kuwa na timu za watoto na vijana ambao baadaye
watakuwa hazina ya Taifa Stars.
Kuhusiana na uvumi ulioenea
kuwa anataka kwenda kufundisha timu za Taifa Stars, Azam na Yanga
alisema kuwa siyo kweli na wala hajawasiliana na timu hizo na hawezi kwenda
kufundisha kwani hivi sasa anamkataba wa kufundisha timu ya
Democrata iliyopo nchini humo.
Rais alimshukuru Kocha Maximo
kwa kuja kumsalimia na kumpa zawadi ya jezi ya timu ya Democrata anayofundisha,
na kumtakia heri na fanaka katika kazi yake hiyo.
“Timu ya Taifa Star ina
kocha mzuri ambaye ninamuheshimu na ninaukubali ufundishaji wake hivyo basi
kupitia kocha huyo ninaamini watanzania watazidi kuendelea katika soka na
kufika mbali zaidi”, alisema.
Maximo alimalizia kwa
kusema kuwa anamawasiliano mazuri na watanzania na anawapenda ndiyo
maana kila mahali anapopita anajivuna na kusema kuwa Tanzania ni
nchi yake ya pili.
Hivi sasa Maximo ni kocha wa
timu ya Democrata iliyopo nchini humo ambapo wiki ijayo inatarajia
kuanza mashindano ya taifa yatakayopelekea kupata wachezaji bora watakaoshiriki
mashindano ya kombe la Dunia yanayotarajia kufanyika mwaka 2014 nchini Brazil.
No comments:
Post a Comment