Steven Kanumba afariki dunia
Mwigizaji STEVEN KANUMBA amefariki dunia na inaaminika chanzo cha kifo
chake ni baada ya kuanguka na kuanza kutoa mapovu hapohapo nyumbani kwake,
alikua akiishi na mdogo wake anaitwa Fetty aliekua chumba kingine ambae
amethibitisha kweli kwamba alimkuta kaka yake akiwa ameanguka.
Polisi wameondoka nyumbani kwa Kanumba baada ya kuwachukua waliokua
wanaishi na Kanumba akiwemo mdogo wake Fetty ili kwenda kusaidia maelezo ya
kilichotokea.
Bado watu wanazidi kuongezeka nyumbani kwa Kanumba ambapo tayari idadi
kubwa ya wasanii wenzake wamefuka pamoja na watu mbalimbali.
Ila kumekua na taarifa nyingine ambazo hazijathibitishwa kwamba Kanumba
alianguka na kuumia kichwani baada ya mpenzi wake ambae anatajwa kuwa ni
mwigizaji LULU kumsukuma na kuanguka wakati wanagombana.
‘Inasemekana’ Kanumba wakati akijiandaa kutoka saa sita usiku aliingia
bafuni kuoga, alipotoka alimkuta Lulu akiongea na mwanaume mwingine kwenye simu
ndipo alipokasirika na ugomvi kuanza.
No comments:
Post a Comment