TAFAKARI...! CHUKUA HATUA!!
Hivi tunawezaje kuishi kwa matumizi yafuatayo kila mwezi?
Hivi tunawezaje kuishi kwa matumizi yafuatayo kila mwezi?
- Matumizi nyumbani;
- Chakula,
- Umeme,
- Gesi,
- Maji,
- Soda/juisi za wageni
- Ada za watoto zinazolingana na za chuo kikuu
- Matibabu hospitalini,
- pesa ya walinzi kwa mwezi,
- sherehe za kuaga na kukaribisha mwaka mpya,
- Zaka ya kanisani na misikitini
- Kupanda Mbegu/ Sadaka Shukurani ya Neno
- Tozo za flying (wazoa taka wa mikokoteni ambao huzitupa hapo hapo)
- Madalali wa nyumba/viwanja
- Pango la nyumba
- Fremu ya biashara/ofisi
- Mazakayo wa mitandao ya simu [airtime vouchers]
- Mafuta ya gari
- Walinda/waosha magari (oya sista/blaza, mdogo wako nipo apaaa)
- Tozo za kuegesha magari
- Makato ya Mikopo
- Tozo za internet cafe ili uweze ku-surf
- Rambirambi ya mfiwa mtaani au ndugu
- Michango ya harusi/send off/kitchen party ya ndugu au rafiki
- Zawadi ya harusi/ sendoff/kitchen party
- zawadi ya kumuaga mfanyakazi mwenzenu
- zawadi michango ya komunio ya 1 & 2 na kipaimara na birthday
- Michango ya birthday party na zawadi ndugu wa kule kijijini
- Mshahara wa Hausigeli na na hausiboi
- Bodaboda,
- teksi na bajaj
- Duka la dawa
- Tuisheni ya mtoto
- Kuchangia wahanga wa mabomu, mafuriko na vistula.
- Kwenda kumuona mtoto aliyezaliwa,
- Kununua CD/DVD ya Uzinduzi wa Kwaya yetu
- Chakula cha mbwa
- Machango wa Ujenzi wa Kupanua Kanisa
- Kuchangia Uinjilisti Masasi /DRC
- Auting ya kitimoto
- Ujenzi wa Nyumba Mwabepande
- Kuendeleza shamba mkuranga (linalotaka kutaifishwa kwa kutoendelezwa)
- Kwa wale wenzetu wanaokwenda umbali wa Viti Virefu, moja moto moja baridi
- Maji ya Traffik
- Chai ya Nesi na Daktari,
- Kahawa ya Hakimu, Karani na PP
- Vishoka waunganisha maji na umeme
- Kidogodogo cha mjumbe na mtendaji wa mtaa
- Mia mbili ya watoto wa mtaani/ombaomba,
- kitu kidogo cha wale wanaolazimisha kuosha kioo cha gari kwenye foleni.
- umeme na gesi vilivyopanda bei,
- maji yaliyoadimika,
- bado contingency maana huu usafiri unaotembelea ball joint,bush,fen belt havijafa...bado service,
- bado msosi wa mchana kazini esp kama maofisi yetu mama ntilie wanakaribiana bei na restaurants
- sare,baby show...
- bado hujatoa watoto outing jumapili n.k
- Kutunza wazazi/Wakwe
- Kuchangia ujenzi wa barabara/zahanati nyumbani utokako na mjini uishipo nk....nk
Hapo mwajiri amekuongezea mshahara kwa 7% tu wakati inflation ni above 19%. Ndipo unapoimba "...Mwokozi nitoe roho niepuke hili balaaa..."
Ukifikiria
kwa makini unajiuliza watanzania wanasurvive vipi kwa style hii???
Imeletwa kwenye blogu toka Tanzanet (www.tanzanet.org)
No comments:
Post a Comment