NIDA yafichua mbinu za
matapeli
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dickson Maimu, amesisitiza kuwa fomu kwa ajili
ya kupatiwa vitambulishio vya taifa haziuzwi na wanaofanya hivyo waripotiwe ili
hatua za kisheria dhidi yao zichukuliwe.
Kwa mujibu wa Maimu, vitendo hivyo
vinalenga kuwahadaa wananchi. Amewataka wananchi kuwa waangalifu na kuwafichua
wanaojihusisha na uuzaji huo wa fomu hizo, ambao ni kinyume cha taratibu,
kanuni na sheria ya usajili.
“Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
(NIDA), haijaanza kutoa fomu zozote za usajili kwa wananchi wa mikoani, zaidi
ya mazoezi ya usajili kwa watumishi wa umma kwa Dar es Salaam na Zanzibar na
zoezi la majaribio Wilaya ya Kilombero, Morogoro lililofanyika Machi,
mwaka huu. Usajili rasmi wa wananchi kwa jumla unakusudiwa kuanza mapema Juni
mwaka huu, kwa kuanzia na Mkoa wa Dar es Salaam.”
Kutoka Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment