Dkt.
Ulimboka azungumza kilichompata
Mwenyekiti wa Jumuia ya Madaktari
nchini Dk Stephen Ulimboka, amepigwa na kujeruhiwa vibaya na watu
wasiofahamika.
Dkt Ulimboka anadaiwa kuvunjwa mbavu,
miguu yote miwili, kung’olewa meno yote ya mbele na kuumizwa vibaya katika
sehemu mbalimbali za mwili wake.
Tukio hilo la kikatili na kusikitisha
limetokea usiku wa kuamkia leo jijini Dar es Salaam, na linadaiwa kufanywa na
watu wa sio julikana ambapo kabla ya kufanya unyama huo walidaiwa kumteka na
kumpiga kabla ya kumtelekeza katika eneo la msitu wa Pande Mabwepande.
DKT. ULIMBOKA ASIMULIA TUKIO
Akisumulia tukio hilo Dkt Ulimboka
alisema kuwa jana usiku alipigiwa simu na mtu aliyejitambulusha kwake
kuwa anaitwa Hemed, aliyemwambia kuwa anahitaji kuongea naye, na ndipo
walipopanga kuonana katika eneo la Leaders Kinondoni.
Dk Ulimboka aliyekuwa akiongea kwa
tabu, aliendelea kusimulia kuwa wakati akiongea na mtu huyo anayekiri kuwa
alikuwa akifahamiana naye kabla, alikuwa na wasiwasi kwani kila mara alikuwa
akipokea simu na kuwasiliana na watu wengine ambao hawakuwapo eneo hilo.
Alisema baada ya muda alishangaa kuona
wanaongezeka watu wengine watano wakiwa na silaha, kisha wakamwambia kuwa
anahitajika kituo cha Polisi na kumvuta na kumuangusha barabarani kabla ya
kumuingiza katika gari lenye rangi nyeusi na kuondoka naye.
Dkt Ulimboka alisema kuwa wakiwa
njiani walimpiga, na kumfikisha katika msitu huo wa pande na kuendelea kumpiga
paka alipoteza fahamu.
MADAKTARI NAO WALONGA
Akisimulia mkasa huo mmoja wa
madaktari wenzie aliyefahamika kwa jina moja la Dkt Deo, alisema kuwa alipigiwa
simu na mtu hasiyemfahamu na kumfahamisha tukio hilo.
Alisema alipofika katika kituo cha
Polisi cha Bunju, alimkuta akiwa katika hali mbaya na ilikuwa ngumu kumtambua
kwakuwa alikuwa na majeraha mengi eneo la usoni.
Aliongeza kuwa akiwa na wenzie
waliamua kumchukua na kumkimbiza katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwaajili
ya matibabu.
"Hali yake kwakweli ni mbaya
sana, amepigwa mno na ameumizwa kwakweli tumemleta hapa hili aweze kupata
matibabu, lakini mimi nilivyomkuta mara ya kwanza nilishindwa hata kumtambua
kwa jinsi alivyokuwa ameumizwa"alisema Dkt Deo
Alisema kuwa alisimuliwa na Dkt
Ulimboka kwamba watu hao waliomteka na kumpiga walikuwa na silaha na kwamba
alishindwa kuwatambua.
Aliongeza kuwa Dkt Ulimboka alidai
kuwa wakati akiwa katika halimbaya alikuwa akisikia mazungumzo yao, wakibishana
juu ya kumuua wengine wakisisitiza achomwe sindano, na wengine wakitaka kumpiga
risasi.
Alisema wakati mabishano yakiendelea
kati yao, Dkt Ulimboka aliinuka akiwa na lengo la kukimbia lakini watu hao
walipiga risasi hewani iliyomshtua na kuangua chini.
Kwa upande wake Dkt Cathbeth Mcharo
ambaye ndiye aliyempokea Dkt Ulimboka Hospitalini hapo, alisema kuwa hali yake
ni mbaya na kwamba wanajitahidi kumpatia huduma za haraka.
Alisema kuwa kwa hatua za awali
amefanyiwa vipimo mbalimbali, hili iweze kufahamika aina ya matibabu
anayotakiwa kupatiwa.
POLISI
Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar
es salaam Kamanda Suleiman Kova amezungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio
hilo la utekaji nyara na kujeruhi lililompata kiongozi mgomo wa Madaktari
Steven Ulimboka anayedaiwa kutekwa na watu watano wakati akipata kinwaji katika
klabu ya Leaders Kiondoni jijini Dar es salaam.
Kamanda Kova amesema Ulimboka
aliokotwa na msamaria mwema ambaye hakutaka kumtaja jina lake kiusalama na
kutoharibu upelelezi kuwa msamaria mwema huyo alimuokota Ulimboka katika msitu
wa Mabwepande na kutoa taarifa kituo cha polisi cha Bunju, ambapo polisi
aliyekuwa zamu alichukua maelezo yake na baadae Steven Ulimboka kuletwa katika
hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Kamanda Kova amesema jeshi la Polisi
Kanda Maalum limeunda jopo maalum kwa ajili ya uchunguzi na upelelezi wa tukio
hilo la utekaji nyara, kwani ni tukio la kwanza kutoke nchini, ameongeza kwamba
wahusika wote watakaobainika kuhusika na tukio hilo wachukuliwa hatua za
kisheria na sheria itafuata mkondo wake ili kukomesha matukio mengine kama hayo
MUHIMBILI
Wakati hayo yakitokea inadaiwa kuwa
Askari Kanzu mmoja alikumbana na kipigo kikali kutoka kwa madaktari hapo
Muhimbili kwa kile kilochodaiwa kutambuliwa na Dkt Ulimboka kuwa mmoja wa watu
walio mjeruhi.
Pia inadaiwa kuwa Askari huyo aliingia
chooni na kufanya mawasiliano na wenzake huku Madaktari hao wakimsikiliza na
kutokana na alichokua akiongea chooni humo ndipo alipotoka aliambulia kichapo
kikali.
Pia baadhi ya madkatari na wauguzi
walikuwa wakisukuma gari alilokuwa amepanda Dkt Ulimboka huku wakiimba nyimbo
za Umoja na Mshikamano Daima miongoni mwao.
Hali ya ulinzi ilikuwa kali
Hospitalini hapo kwani Picha zilikuwa haziruhusiwi kupigwa.
No comments:
Post a Comment