Tanzania yamkamata Erdogan
Mtu mmoja anayeshukiwa kuwa ana uhusiano na shambulio la mwezi uliopita
katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi amekamatwa nchini Tanzania.
Polisi ya Kenya inasema kuwa Emrah
Erdogan ni raia wa Ujerumani mwenye asili ya Uturuki.
Kenya inadai kuwa alivuka mpaka
mapema mwezi Mayi kutoka Somalia ambako alishiriki mapigano kwa niaba ya kundi
la Al Shabab.
Zaidi ya watu 30 walijeruhiwa katika
mlipuko ambao wakuu wa Kenya wanasema ulisababishwa na bomu hilo.
Kumekuepo na sintofahamu juu ya
chanzo cha mlipuko huo- ambapo Maofisa wa Polisi walianza kwa kusema kuwa
mlipuko huo ulisababishwa na hitilafu ya umeme.
Mara kwa mara kundi la Al Shabab
limetishia kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi nchini Kenya kwa sababu nchi
hio ilituma vikosi nchini Somalia.
Serikali ya Kenya inalituhumu kundi
la wapiganaji wa Al Shabab kuhusiana na utekaji nyara wa watu kadhaa kwenye
ardhi yake pamoja na kusababisha hali ya wasiwasi kwenye mpaka baina yake na
Somalia.
Polisi ya Tanzania imethibitisha kwa
BBC kuwa Bw.Erdogan alikamatwa na kuahidi maelezo zaidi baadaya mda mfupi.
Erdogan ni miongoni mwa watu wanne
ambao Polisi ya Kenya imekua ikiwasaka tangu kutokea kwa mlipuko huo.
Ilisambaza picha yake na kuomba
habari kuhusu mahali alipo.
Bw.Erdogan, anayejulikana pia kama
Salahuddin al-Kurdi, inaaminika kuwa aliwahi kusafiri kwenda Waziristan huko
Pakistan ya kaskazini magharibi mwaka 2010 ambako alijiunga na kundi la
wakereketwa wenye imani kali kabla ya kuelekea Somalia mwaka jana, kwa mujibu
wa shirika la habari Reuters.
Mapema mwaka huu, vikosi vya AU
vinavyounga mkono serikali ya mseto nchini Somalia viliongezea idadi ya askari
wake kutoka 12,000 hadi 18,000 kujumuisha vikosi vya Kenya vilivyoingia nchi
hio mnamo mwezi Oktoba mwaka jana kuwasaka wapiganaji wa Al Shabab.
Kundi la Al-Shabab, lililojiunga na
mtandao wa al-Qaeda mapema mwaka huu imefahamika lilisajili wapiganaji wa
kigeni kadhaa -wengi ambao wamewahi kupigana huko Iraq na Afghanistan.
Kutoka BBC Kiswahili
No comments:
Post a Comment