Mauaji ya balozi
yachunguzwa Kenya
Marehemu Olga Fonseca
Polisi wa Kenya wanasema kuwa
wanaendelea na uchunguzi, juu ya mauaji ya balozi mpya wa Venezuela nchini
humo, ambaye aliuwawa Ijumaa.
Olga Fonseca, aliyeanza kazi Kenya kati ya mwezi Julai,
alikutiakana ameuwawa nyumbani kwake, na watu sita wamekamatwa hadi sasa.
Watu hao sita wamekamatwa siku mbili tu baada ya balozi huyo
kupatikana amefariki nyumbani kwake.
Siku ya Ijumaa, polisi walisema kuwa maiti ya Bi Olga Fonseca
ilipatikana kitandani mwake lakini sababu za kuuwawa kwake hadi sasa
hazijulikani.
Bila ya kutoa
maelezo zaidi, polisi wamesema kuwa wanawashikilia watu sita kuhusiana na kifo
cha balozi huyo.
Taarifa kutoka
wizara ya maswala ya njee ya Kenya imesema kuwa wafanyikazi katika makaazi ya
balozi huyo waliwasilisha malalamiko yao kwa polisi baada ya kufutwa kazi hivi
majuzi.
Inadaiwa kuwa
bi Fonseca aliwafuta kazi baada ya wao kukataa kuondoa malalamiko kuhusu madai
ya kunyanyaswa kijinisia na mtangulizi wa balozi huo.
Hata hivyo polisi wamesema wanachunguza madai hyao.
Chanzo: BBC
Kiswahili
No comments:
Post a Comment