TAMKO RASMI KUHUSU TUHUMA DHIDI YA IDARA YA USALAMA WA TAIFA
Katika siku za hivi karibuni,
kumejitokeza taarifa zenye tuhuma kadhaa dhidi ya Idara ya Usalama wa Taifa.
Taarifa hizo zimekuwa zikitolewa kwenye vyombo vya habari zikiihusisha Idara
hii na matukio ambayo yanaidhalilisha na kuzua maswali mengi kwa wananchi.
Kati ya tuhuma hizo ni tukio
la kutekwa kwa Dr. STEPHEN ULIMBOKA, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari na
madai ya kufanywa kwa mipango ya kuwadhuru baadhi ya Viongozi wa Vyama vya
Upinzani. Gazeti moja la kila wiki limekuwa likurudia tuhuma hizo mara kwa mara
kwa madai kwamba ni habari za uchunguzi na kuihusisha Idara.
Idara inataka kuwahakikishia
wananchi kwamba taarifa hizo ni za UZUSHI NA UONGO ambazo zina
nia ya kuharibu jina na sifa ya Idara. Taarifa hizo zimekuwa
zikiunganishaunganisha vipande vya taarifa mbalimbali ili kukidhi malengo
yaliyokusudiwa na wanaolitumia gazeti hilo. Idara haikuhusika wala haihusiki na
matukio yoyote yaliyotajwa katika tuhuma hizo.
Hivyo tunawaomba wananchi wazipuuze
taarifa hizo. Matukio yaliyotajwa katika tuhuma hizo yanachunguzwa na Jeshi la
Polisi ambacho ndicho Chombo Chenye Dhamana, na kwa Maslahi ya Taifa si vizuri
kuachia upotoshaji huo uendelee.
Aidha, tunapenda kuwahakikishia Watanzania kuwa uzushi na tuhuma zinazotolewa dhidi ya Idara hazitatuvunja moyo bali zitatuunganisha na hivyo kutuimarisha katika azma yetu ya kuhakikisha nchi yetu inaendelea kubaki salama kwa kushirikiana na wanachi na Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama.
Imetolewa na

Idara ya Usalama wa Taifa,
Makao Makuu,
DAR ES SALAAM
26 Julai, 2012.
No comments:
Post a Comment