Kashfa
ya mabilioni kufichwa Uswisi, Watanzania 27 wahusika. Mmoja anamiliki
shs.bilioni 90, wengine wanne wameficha shs.bilioni 112
WATANZANIA
27 wakiwamo wanasiasa na wafanyabiashara, imebainika kuwa ndiyo wameficha
mabilioni ya fedha nchini Uswisi, huku mmoja wao akiwa anamiliki Dola za
Marekani milioni 56 (sawa na Sh89.6 bilioni).Katika uchunguzi wake, Mwananchi
imebaini pia kuwa kiasi cha fedha kilichothibitishwa kumilikiwa na Watanzania
hao ni jumla ya Dola za Marekani 186 milioni (Karibu Sh300 bilioni) kwa viwango
vya sasa vya kubadilishia fedha ambavyo ni Sh1600 kwa Dola ya Marekani.
Taarifa
hizo zinaeleza kuwa mbali na kigogo anayemiliki Sh90 bilioni, wapo wengine
wanne, ambapo anayefuatia anamiliki Dola 30 milioni (Sh48 bilioni), mwingine
Dola 20 milioni (Sh32 bilioni) na wengine wawili kila mmoja anamiliki Dola 10
milioni (Sh16 bilioni). Kwa kuangalia fedha hizo ni
dhahiri kwamba vigogo watano tu kati ya kundi la Watanzania 27, wanamiliki Dola
126 milioni (Sh201.6 bilioni) sawa na asilimia 67.74 ya fedha hizo, wakati
wengine 22 waliobaki wanamiliki Dola 60 milioni (Sh96 bilioni) sawa na asilimia
32.25.
Kwa
hesabu za kawaida, kiasi cha Sh300 bilioni, kinaweza kugharimia ujenzi wa
vyumba vya madarasa zaidi ya 33,300, ikiwa chumba kimoja kinaghirimu kiasi cha
Sh9 milioni.
Katika
orodha ya walioweka fedha nchini humo, pia wamo wafanyabiashara wanaomiliki
kiasi cha dola kati ya milioni mbili na milioni saba. Kadhalika wamo wawili
waliowahi kuwa mawaziri katika Serikali ya Awamu ya Kwanza ya Mwalimu Julius
Nyerere, ambao akaunti zao zina kiasi kisichozidi Dola 500,000 kwa kila mmoja.
Kashfa ya
kuwapo kwa vigogo walioficha fedha zao nchini Uswisi iliibuliwa na baadhi ya vyombo
vya habari nchini mwezi Juni mwaka huu, na baadaye mwangwi wake kulitikisa
Bunge katika mkutano wake wa nane uliomalizika juzi mjini Dodoma.
Habari
hizo zilikuwa zikinukuu taarifa ya Benki Kuu ya Uswisi iliyoitoa na kuonyesha
kuwapo kwa kiasi cha Sh315.5 bilioni zilizotoroshwa Tanzania na kufichwa nchini
humo na vigogo ambao ni wanasiasa pamoja na wafanyabiashara.
Jumatano
wiki hii, tuhuma hizo ziliibuka bungeni ambapo Kambi ya Upinzani ilidai kwamba
inawafahamu wahusika wa ufisadi huo na kutishia kuwataja ikiwa Serikali
haitawataja.
Naibu
Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe alipokuwa akiwasilisha hotuba ya
kambi yake kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Fedha na Uchumi alisema,
miongoni mwa wanaomiliki fedha hizo ni kiongozi wa juu nchini pamoja na
aliyepata kuwa waziri katika Serikali ya Awamu ya Tatu iliyoongozwa na Rais
Benjamin Mkapa.
“Kambi ya
Upinzani bungeni imepata taarifa mmoja wa viongozi wa juu kabisa wa Tanzania na
baadhi ya mawaziri wa awamu zilizopita ni miongoni mwa watu wenye fedha hizi,”
alisema Zitto huku akiitaka Serikali kuliambia taifa ni hatua gani
itakazochukua kurejesha fedha hizo pia kuwataja wamiliki wake.
Baada ya
Zitto kumaliza kuwasilisha hotuba yake, Mbunge wa Simanjiro (CCM), Christopher
Ole-Sendeka aliomba mwongozo wa Spika kuhusu suala hilo, akisema kuwa tuhuma
hizo ni nzito, hivyo kumwomba Naibu Spika, Job Ndugai amtake kutoa ufafanuzi
ama ikiwezekana kuwataja wahusika.
Hata
hivyo, Ndugai baadaye alisema taarifa hizo ni za uongo na uzushi kwani Zitto
hakuwa na ushahidi wa kuthibitisha kauli yake wala kuwataja wahusika kama
ambavyo alidai, huku akimtuhumu kwamba anautumia vibaya Ukumbi wa Bunge kwa
kutoa tuhuma nzito bila kuzifanyia utafiti.
Uchunguzi
zaidi Katika hotuba yake bungeni, Zitto alidai kuwa fedha hizo
zinatokana na biashara (deals) zilizofanywa na watendaji wa Serikali na
wafanyabiashara kwenye sekta za nishati na madini na kwamba sehemu kubwa ya
fedha zililipwa na kampuni za utafutaji mafuta na gesi katika Pwani ya Mkoa wa
Mtwara zilizopewa mikataba kati ya mwaka 2004 na 2006.
Hata
hivyo, uchunguzi zaidi wa gazeti hili umebaini kuwa fedha zilizopo kwenye
akaunti za vigogo wanaohusishwa na ufisadi huo, mara ya mwisho ziliwekwa kwenye
akaunti husika mwaka 2005.
Taarifa
zaidi ambazo Mwananchi limezipata zinadai kuwa taarifa za kufichwa kwa
mabilioni hayo ya shilingi nchini Uswisi zimekuwa zikipatikana kwa msaada wa
Mbunge mmoja wa zamani wa Afrika Kusini, (jina tunalihifadhi kwa sasa).
Akizungumza jana Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema) anasisitiza kuwa walioweka fedha hizo nchini Uswisi wanafahamika na kwamba ikiwa Serikali haitawataja na kuwachukulia hatua, wao (Chadema) watawataja wakati mwafaka ukifika.
Akizungumza jana Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema) anasisitiza kuwa walioweka fedha hizo nchini Uswisi wanafahamika na kwamba ikiwa Serikali haitawataja na kuwachukulia hatua, wao (Chadema) watawataja wakati mwafaka ukifika.
“Kama
nlivyowahi kusema, tufanye kama nchi ya India, wenzetu hawa walitangaza
kwamba watu wote walioweka fedha nje ya nchi kwa njia isiyo halali,
wazirejeshe. Walifanikiwa sana, na sisi tunapaswa kufuata nyayo hizo, fedha
hizo tunazitaka ili zitusaidie katika kuendesha uchumi wetu,” alisema Zitto.
Chanzo: Mwananchi
No comments:
Post a Comment