Mwalimu
afukuzwa kazi kwa kuzungumza Kiswahili, Arusha.
Ninaomba WIZARA YA ELIMU iwe makini na
wawekezaji katika secta ya elimu, hasa kwenye shule ambazo zinatoa msaada kwa
watoto wakitanzania ambao familia zao hazina uwezo wa kifedha, kwa mfano
ninaomba mmiliki wa shule ya St Jude apate muda wa kusikiliza kilio cha
wafanyakazi wake wakitanzania kwani kimsingi wamekuwa wakiteswa, kukandamizwa
na kupuuzwa wanapodai haki na maslahi bora kazini kwao.
Mwalimu Daniel Urioh |
Shule hii utumia picha za wafanyakazi kuzalisha kiasi kikubwa cha fedha
kuendesha shule, kwa wafanyakazi na wanafunzi hupigwa picha mara kwa mara na
kulazimishwa kuleta picha za familia zao kila mwaka bila shule kuweka wazi kwa
mfanyakazi kuwa anawafadhili wangapi, wafadhili huchangia kiasi gani cha
fedha, kukatazwa kuwasiliana na mfadhili, kuruhusiwa kuhoji lolote kuhusu pato
na matumizi ya uzalishwaji wa fedha kupitia wewe na familia yako? Hata hivyo
picha za familia zinazalisha fedha kwaajili ya uendeshaji wa shule ilihali
familia haifaidiki kwa uuzaji huo wa sura zao ughaibuni? Kinachosikitisha zidi
ni pale mfanyakazi anapoachishwa ,shule inaendelea kitumia picha za wafanya
kazi na familia zao kuzalisha fedha nyingi za kigeni bila ridhaa wala fedha
hizo kuwafaidisha wenye picha, na kutojali kuwa kitendo hicho kinyume na
sheria.
Pia picha hizo zimekuwa mara kadhaa zikidhalilisha utu na uhuru wa
muafrika, kwani sura za watanzania zimekuwa bidhaa ya kuzalisha fedha
zisizojulikana ni kiasi gani na kwa faida ya nani? tena ulazimisha vitendo
visivyo halisi na maisha yetu mfano unalazimishwa kucheka ukichukuliwa picha
ilihali mapato uzalishayo hujui na ukikataa kutekeleza unatishiwa kufukuzwa
kazi, wanafunzi ushikishwa zawadi zisikuwa zao na kupigwa picha na uzalisha
kiasi cha fedha bila ridhaa wafunzi wanapohoji hupewa adhabu au kutishiwa
kufukuzwa.
Kama hiyo aitoshi shule hii imekuwa mara kadhaa ikipuuza sheria za nchi
bila sababu za msingi mfano wamekuwa wakiajiri familia za ughaibuni kinyume na
sheria za nchi mfano wanaajiri baba, mama na mtoto wa familia moja tena kwenye
nafasi za juu na kutoweka wazi taaluma zao wakiwaaminisha kuwa ukiwa mzungu
basi we msomi wa kila kitu, kinyume na sheria ya ajira nchini, pia shule
imekuwa mara kadhaa haieshimu sikukuu za kitaifa bila sababu za lazima na
kutojali wala kuthamini mchango wa waasisi na wazalendo waliopoteza maisha
kujenga utaifa, amani na umoja wa Tanzania, cha kushangaza shule ujiamulia siku
za mapumziko ya wafanyakazi na wanafunzi watakavyo wao, huwa najiuliza
hivi shida inaweza tulazimisha kufuata sheria za wawekezaji na kupuuza
sheria za nchi yetu Tanzania?
Linalosikitisha
zaidi shule hii imekuwa hodari wa kupiga vita ya matumizi ya lugha ya
kishwahili kwa wanafunzi na wafanyakazi hata kudiriki kuwaadhibu kwa
kuwarudisha wanafunzi nyumbani kwa kosa la kuzunguza kishwahili, hata kufika
mbali zaidi na kufukuza mwalimu mwenye shahada ya ualimu kwa kosa ni kuzungumza
kishwahili na wanafunzi, huu ni uvunjaji wa sheria za nchi usiovumilika.
Hata hivyo nataka
wao wajue kuwa lugha ya taifa Kiswahili imekuwa mhimili mkubwa wa kujenga umoja
na amani. Kiasi cha kuwa wekeza kupata mafanikio, kama awa amini wakajaribu
kuwekeza Somalia na kuwasaidie watoto wa Somalia wenye shida kubwa ya elimu,
ilo linge ondoa jeuri yao ya kupuuza sheria za Tanzania.
Kitendo cha shule
hii kuwatumia watanzania kama bidhaa na utaratibu wao wa fukuza fukuza
waliyonayo hasa kwa watanzania. Shule hii huwatumia viongozi wazalendo
kuwanyanyasa wenzao na kusaidia shule kuendelea na dharau na kupuuza
sheria za nchi zenye maslahi kwa wazalendo, wale wote watakaonyesha uzalendo
kama mimi wakuonyesha kukerwa na kuchukua hatua ya kuhoji na kutetea sheria za
nchi na watanzania dhidi ya upuuzwaji wa uzalendo, haki, utu, lugha ya taifa,
maslahi ya kiwango cha utumikishwaji, niliishia kufukuzwa kwa kosa la kuongea
kishahili na wanafunzi.
Ushauri wangu kwa
wizara ya elimu.
Kwanza kupandisha
mshahara na mazingira ya kazi serikalini ilikuvutia waalimu wote toka shule
binafsi kwani wangi wamechoshwa ni manyanyaso ya waajiri.
Pili kufanya
ukagua si wa taaluma tu bali pia mfumo wa uajiri na maslahi ya watanzania
waajiriwa kwenye shule zinazomilikiwa binafsi kwa misaada ya watu toka
ughaibuni.
Tatu iwe na
utaratibu wa ufuatiliaji wa mapato na matumizi ya shule zinazopata fedha toka
kwa wafadhili kwani shida za watanzania zimekuwa zikinufaisha wachache na
kutengeneza ajira ya watu wasiona sifa za kufanya kazi ughaibuni na kuja
kufanya kazi ambazo wazalendo wanaweza kuzifanya.
Nne kusisitiza
hasa shule binafsi nchini kuthamini lugha ya kishwahili, kuheshimu sheria za
ajira, kuheshimu sikukuu za kitaifa na kuheshimu, kulinda tamaduni na
vipaji vya watanzania kwa manufaa ya Tanzania.
Ni kweli tar
15/06/2012 nimefukuzwa kazi ya kufundisha (ualimu) St-Jude-Arusha kwa kosa la
kuzungumza Kiswahili.
Uzalendo gharama
nimeamua kujitoa kwa kutetea nchi yangu Tanzania.
Mwalimu Daniel
Urioh. Kwa undani zaidi piga : +255 755 379 737
No comments:
Post a Comment