Luteni
Jenerali Ndomba, Mnadhimu Mkuu mpya wa JWTZ
Mnadhimu Mkuu mpya wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Meja
Jenerali Samwel Ndomba akila kiapo mbele ya Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya
Ulinzi na Usalama, Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri
Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Meja Jenerali Samuel
Albert Ndomba kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Aidha, Rais Kikwete amempandisha cheo Meja Jenerali
Ndomba kuwa Luteni Jenerali.
Taarifa iliyotolewa leo, Ijumaa, Septemba 21,
2012, mjini Dar Es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue
kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais – Ikulu, imesema kuwa uteuzi huo
unaanza leo.
Taarifa hiyo ya Balozi Sefue imesema kuwa kabla ya
uteuzi wake, Meja Jenerali Ndomba alikuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Jenerali Ndomba anachukua nafasi iliyoachwa wazi
na Luteni Jenerali Abdulrahman A. Shimbo
ambaye amestaafu Jeshi kwa mujibu wa sheria baada ya kufikisha umri wa miaka
60.
Taarifa ya Balozi Sefue pia imesema kuwa Rais
Kikwete amemteua Brigedia Jenerali Raphael Mugoya Muhuga kuwa Mkuu wa Jeshi la
Kujenga Taifa kuanzia leo, Ijumaa, Septemba 21, 2012.
Aidha, Rais Kikwete amempandisha cheo Brigedia
Jenerali Muhuga kuwa Meja Jenerali.
Kabla ya uteuzi wake, Brigedia Jenerali Muhuga
alikuwa Mkuu wa Utawala na Mafunzo wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Imetolewa na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
21 Septemba, 2012
No comments:
Post a Comment