Friday, September 07, 2012

Tamko la awali la serikali juu ya risala ya Waislam kwa mheshimiwa waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Mambo ya Ndani ya Nchi tarehe 7.Septemba, 2012


1. Kutokana na mheshimiwa waziri na naibu wake kuwa nje ya ofisi, katibu mkuu wa wizara ya mambo ya ndani ya nchi amepokea risala ya waislamu na kwamba ataifikisha kwa waziri mara tu atakaporudi nchini.

2. Katika mazungumzo kuna maneno kuwa kuna waislamu wamewekwa ndani kutokana na zoezi linaloendelea la sensa.  katibu mkuu wa wizara ya mambo ya ndani ya nchi, ametoa amri kwa rpc wote kusitisha ukamataji wa watu kutokana na zoezi la sensa na kwamba watuhumiwa waliokamatwa waachiwe kwa dhamana.

3. Mambo mengine yote yaliyotajwa kwenye risala ya waislamu yatashughulikiwa mara baada ya waheshimiwa mawaziri wenye dhamana hiyo kurudi na mtajulishwa.
Tamko limetolewa na,

Mbarak M. Abdulwakil
Katibu Mkuu
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
7.Septemba, 2012
Usuli: Leo tarehe 07 majira ya alasiri, baadhi ya waumini wa madhehebu ya Kiislamu waliandamana hadi Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakiwa na hoja mbalimbali ambazo waliziandika kama Risala kwa lengo la kuziwasilisha kwa Waziri wa Mambo  ya Ndani ya Nchi.  Hata hivyo Waziri na Naibu wake wako safarini hivyo Risala hiyo ilipokelewa na Katibu Mkuu wa Wizara, Mbarak Abdulwakil, ambaye baada ya majadiliano alitoa tamko hili hapa juu kwa niaba ya Waziri.

(Imesambazwa na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

No comments: