Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametangaza kuwa kesho,
Jumatatu, Januari 13, 2014, itakuwa ni Siku ya Mapumziko kwa Watanzania wote
kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais Kikwete
ameutangaza uamuzi huo mjini Zanzibar ambako leo ameungana na Watanzania na Wazanzibari wote
kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Januari 12, mwaka 1964.
Mapinduzi hayo
yaliyoongozwa na mwasisi wa Zanzibar na Taifa la Tanzania, Hayati
Abeid Amaan Karume yalifanikiwa kuung’oa madarakani utawala dhalimu wa Sultan na
kuwawezesha kwa mara ya kwanza katika historia Waafrika walio wengine kujitawala ndani ya nchi yao wenyewe.
Abeid Amaan Karume yalifanikiwa kuung’oa madarakani utawala dhalimu wa Sultan na
kuwawezesha kwa mara ya kwanza katika historia Waafrika walio wengine kujitawala ndani ya nchi yao wenyewe.
Yalikuwa ni
Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofungua njia ya kuzaliwa kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar – miezi mitatu
baada ya Mapinduzi hayo – Aprili 26, 1964.
Naye Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Ali Mohamed Shein ametangaza kuwa kesho
itakuwa Siku ya Mapumziko Tanzania Visiwani kusheherekea
miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais Shein
alitangaza mapumziko hayo wakati alipohutubia wananchi kwenye Uwanja wa Michezo wa Amaan mjini Zanzibar
katika kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi.
No comments:
Post a Comment