Bi. Itika Kasambala, mshtaki kwenye kesi inayomkabili Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Dkt. Mahongoro Mahanga.
NAIBU Waziri wa Kazi, Ajira na
Maendeleo ya Vijana, Dkt Makongoro Mahanga ameingia kwenye kashfa nzito ya
kuvunja sheria za kazi nchini kwa kumfanyisha kazi msaidizi wake (PS) wa ofisi
yake Bunge kwa miaka kumi bila mkataba na kumlipa fedha taslimu shilingi laki
mbili tu (200,000) kama mafao.
Naibu Waziri, Mahanga anakuwa
kiongozi wa kwanza kuingia kwenye kashfa akiwa madarakani tena kwenye swala la
ajira wakati yeye mwenyewe ni waziri mwenye dhamana na maswala ya ajira na haki
za wafanyakazi nchini chanzo chetu kimeelezwa.
Kwa mujibu wa sheria kazi na
mahusiano kazini, Naibu Waziri amekiuka kifungu cha 3 cha sheria ya Taasisi za
kazi za mwaka 2004 na pia amekiuka sehemu ya tatu ya viwango vya ajira na
sehemu ndogo A kwa kushidwa kuandika mkataba kwa mujibu wa kifungu cha 14 ibara
ya kwanza kama sheria ya kazi na mahusiano kazini inavyotaka.
Katika kifungu hicho cha 14 ibara ya
kwanza kinasema mkataba utakuwa wa kipindi cha muda usiotajwa, mkataba wa kazi
maalumu na mkataba unatakiwa kuwa wa maandishi ambapo vyote Mhe Naibu Waziri
hakufanya.
Ibara ya 15 kifungu cha.-(1)
kinasema kwa kuzingatia masharti ya kifungu kidogo cha (2) cha kifungu cha 19,
mwajiri anatakiwa kumpa mfanyakazi, wakati mfanyakazi anapoanza kazi, taarifa
zifuatazo kwa maandishi, jina, umri, anuani ya kudumu na jinsia ya mfanyakazi;
mahali alipoajiriwa; kazi zake; tarehe ya kuanza; muundo na muda wa mkataba;
kituo cha kazi; masaa ya kazi; ujira na njia ya ukokotoaji wake, na taarifa za
mafao mengine.
Akizungumza na mwandishi wa habari
hizi hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Bi. Itika Kasambala (31) anasema
alianza kazi kwa Mbunge huyo wa Segerea na Naibu Waziri wa kazi Dkt. Mahanga,
mwaka 2003 kama PS (Personal Secretary) kwa makubaliano ya kumpa mshahara wa
shilingi 120,000 kwa mwezi lakini alianza kumlipa shilingi 50,000 tu.
“Aliniambia kwamba nianze kazi
kwanza baadaye atanipa mkataba wa ajira na kunilipa mafao ya hifadhi ya jamii
na matibabu lakini baada ya miaka kumi ananitumia sms akiwa Dodoma kwamba kazi
basi sikuhitaji tena,” Kasambala alisema.
Amesema kwamba Mbunge huyo alimtumia
sms akiwa kwenye vikao vya bunge mjini dodoma mwaka jana mwezi wa sita
akimjulisha kwamba ajira yake imeshafika kikomo kwa sababu hana uwezo tena wa
kumlipa mshahara na mahitaji mengine ya kiofisi.
Kasambala aliendelea kusema kwamba
mara ya kwanza wakati anaanza kazi mwezi wa tano mwaka 2003 baada ya msaidizi
wa ofisi ya mbunge Mahanga kuacha kazi na ndipo alipotafutwa yeye na walikwenda
kuelewana kwa malipo ya 120,000 kwa mwezi.
Alisisitiza kwamba mara baada ya
kuanza kazi kwa ofisi ya mbunge alikuwa analipa pesa kupitia mkononi na baadaye
tigo pesa na baada ya muda akawa anachukua pesa yake ya mshahara toka katika
manisapaa ya Ilala kama posho ya Mhe Mahanga kama diwani kila mwezi.
Dada huyo kwa mshangao baada ya
mahojiano ya muda mrefu alikiri kwamba Mhe Mahanga alikuwa na nia ya dhati
kuanzisha mahusiano ya kimapenzi na kumtaka aende Dodoma lakini alikataa
kufanya masharti hayo.
“Mwaka juzi baada ya kuonyesha nia
ya kunitaka kimapenzi alinipigia simu akitaka niende Dodoma bungeni kwa
mazungumzo zaidi kama msaidizi wake lakini nilikataa,’ aliongeza Kasambala.
Amesema tangu aanze kazi kwa Mhe
Mahanga hakuwa anatoa huduma zozote kama matibabu au fedha kwa ajili ya sikukuu
ilikuwa ni mshahara tu wa 120,000 kwa mwezi lakini kila akimfuata ili
waandikishiane mkataba alikuwa akizungumsha bila sababu za msingi.
Bi Kasambala aliongeza kuwa amefanya
kazi Mhe Mahanga tangu akiwa mbunge wa Ukonga na baadaye Segerea lakini
ameshidwa kuheshimu sheria za ajira na taratibu za kazi wakati yeye mwenyewe ni
waziri mwenye dhamana ya ajira kwa watanzania.
Amesema mwaka jana tarehe 14/09/2013
alimtumia kwa Tigopesa kiasi cha shilingi za Tanzania 200,000 kama mafao yake
baada ya kufanya kazi kwa takribani miaka 10 kama Msaidizi wake wa Ofisi ya
Mbunge.
Amesema kwamba aliamua kwenda Chama
cha Wafanyakazi wa Hifadhi, Mahoteli, Majumbani na Kazi Nyingine (CHODAWU) kwa
msaada wa ksiheria ba baada ya kukutanishwa bado Mhe Mahanga akawa mgumu
kukubaliana kiungwana mpaka ikawalazimu kwenda mahakani Tume ya Usuluhishi na
Upatanishi.
Akizungumza na mwandishi wa habari
hizi wakili wa Kasambala, Nyaisa Godwin alisema kuwa kesi imefunguliwa mahakama
ya kazi wiki iliyopita siku ya Jumanne, Tume ya Usuluhishi na Upatanishi kesi
namba CMA/DSM/ILA/R.711/13.
Wakili Nyaisa alisisitiza kwamba Naibu
Waziri aliiambia mahakama kwamba Dada Kasambala alikuja kufanya kazi kwake kama
mwanafunzi wa chuo kwenye mazoezi lakini alishidwa kuithibitishia mahakama kwa
ushawishi wa barua ya (field to chuoni).
“Tulishagazwa na majibu ya waziri
kwamba dada huyo alikuwa field, na nilimuuliza field ya miaka kumi? Alishidwa
kutoa jibu mbele ya mpatanishi (Arbitrator),” amesema Nyaisa.
Nyaisa aliendelea kusema kutokana na
matatizo ya kuachishwa kazi ghafla bila taratibu dada huyo amepata maradhi ya
presha, vidondo vya tumbo na maradhi mengine baada ya kufanya kazi kwa Mhe
Mbunge kwa miaka kumi bila matibabu wala kulipiwa mifuko ya hifadhi za jamii.
Wakili Nyaisa aliongeza kwamba kesi
hiyo ya aina yake dhidi ya Naibu Waziri wa Kazi itasomwa tena tarehe 13/02/2014
katika Tume ya Usuluhisho na Upatanishi.
Juhudi za kumtafuta, Naibu Waziri wa
Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Dkt. Mahanga hazikuzaa matunda baada ya
simu yake ya kiganjani kushidwa kupatikana kwa muda mrefu alipotafutwa kwa
ajili ya kutoa ufafanuzi.
No comments:
Post a Comment