Mheshimiwa
Mwenyekiti,
Sura ya Kwanza na
Sura ya Sita ya Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (‘Rasimu’)
ndizo msingi ambao Rasimu yote imejengwa juu yao. Wakati Sura ya Kwanza inagusa
suala la muundo wa Muungano katika ibara moja tu kati ya ibara tisa, Sura yote ya
Sita inahusu ‘Muundo wa Jamhuri ya Muungano.’ Suala la Muungano na hasa Muundo
wake limetawala mjadala wa kisiasa na kikatiba wa Tanzania kwa zaidi ya miaka
thelathini. Ndio maana katika waraka wake wa siri kwa Halmashauri Kuu ya Chama
cha Mapinduzi (‘CCM’), Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa ya chama hicho
imetamka kwamba “muundo wa Muungano ndiyo moyo wa Rasimu na ndiyo unaoamua
ibara nyingine zikae vipi.”
Suala hili pia
limetawala mchakato wa Katiba Mpya tangu ulipoanza miaka mitatu iliyopita. Kama
alivyosema Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Joseph Sinde Warioba
wakati wa kuwasilisha Ripoti ya Tume yake kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano na
Rais wa Zanzibar tarehe 30 Disemba, 2013: “Moja ya mambo ambayo yamejadiliwa
sana na kwa hisia kali tangu Rasimu ya awali ilipotolewa ... ni Muungano wa
Tanzania. Jambo kubwa limekuwa juu ya muundo wa Muungano.”...
Bofya na soma
zaidi: http://www.jestina-george.com/hotuba-ya-mh-tundu-lissu-iliyokatishwa
No comments:
Post a Comment