Said Hassan Said Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar
Chanzo: http://www.zanzinews.com
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, amefanya Uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serekali ya Mapinduzi Zanzibar, kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu 55(1)cha Katiba ya Zanzibar ya 1984,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi amemteuwa Mhe, Said Hassan Said kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Uteuzi huo umeaza leo 7,Oktoba 2014. Kabla ya uteuzi huo Mhe, Said Hassan Said alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Mhe, Said Hassan Said, anachukua nafasi ya aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe, Othman Masoud Othman ambaye uteuzi wake umefutwa kwa mujibu wa Vifungu vya 53,54 (1) na 55(3) vya Katiba ya Zanzibar ya 1984 na kifungu 12 (3) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Namba 2 ya 2011.
Chanzo: http://www.zanzinews.com
No comments:
Post a Comment