Friday, June 01, 2007

Uchaguzi mkuu wa Yanga, Jumatano 30 Mei 2007





















"Yanga Daima Mbele Nyuma Mwiko"


1. Mwenyekiti - Imani Madega
2. Makamu mwenyekiti - Rashidi Ngozoma Matunda
3. Katibu mkuu - Lucas Kisasa
4. Katibu mkuu msaidizi - Ahmed Mamba
5. Mhazini - Abeid Mohamed Abeid
6. Msaidizi mhazini - Godfrey Mwenje
7. Katibu mipango - Patrick Fataa
8. Katibu mwenezi - Francis Lucas

Waliogombea walikuwa 51 na wapiga kura walikuwa 1025 kati ya wanachama zaidi ya elfu 5 ambao ni pamoja na wa makundi ya Yanga asili, Kampuni, Bomba na Academia. Vigogo walioshindwa ni pamoja na Baraka Igangula na Kibo Merinyo, Mohamed Bindha na Ismaili Idrisa katika nafasi ya uenyekiti.

Vigogo wengine walioshindwa ni pamoja na Saidi Motisha ambao walianguka katika nafasi ya makamu mwenyekiti, Shabani Dilunga na Patrick Fataa aliyejitoa. Vigogo walioanguka nafasi ya katibu mkuu ni Constantine Maligo na Emmanuel Mpangala. Mchezaji wa zamani wa Yanga Bakari Malima 'Jembe Ulaya' alianguka katika nafasi ya katibu mwenezi.

Katika nafasi ya uhazini baadhi ya vigogo walioanguka ni Castro Mketto, Jeremiah Michael, Paschal Kiyomba na Evarist Mwang'onda aliyejitoa.

Vioja: Pale rais aliyemaliza muda wake Francis Mponjoli Kifukwe alipogoma kwenda kusimamia uhesabuji kura za mgombea wa nafasi ya makamu mwenyekiti Saidi Motisha kwa kile alichodai 'mgombea hana kura za kusimamia', hivyo mgombea akaomba meza kuu imsimamie. Pia wanachama waliinuka kucheza 'mugongomugongo' ya Twanga Pepeta wakati kura zinahesabiwa...

Umbea: Wanachama waliokataliwa kuingia ukumbini kupiga kura walisikika wakiapa kuwa wataenda mahakamani kupinga uchaguzi baada ya kunyimwa haki yao; madai ni kwamba kwa vile ilikuwa ni siku ya kazi pamoja na kuweko na mvua kubwa na foleni ya magari wengi wao walidai kuwa walichelewa kufika kwa sababu hizo...

Chanzo cha habari: Muhidin Issa Michuzi.

Blogu ya WanaYanga: http://yangatz.blogspot.com/

No comments: