Wednesday, December 12, 2018
Kwa Watanzania na wenye nasaba na asili ya Tanzania duniani


Tunapenda kukujulisha kuwepo kwa Baraza la Diaspora kwa Watanzania Duniani. Lengo la Baraza ni kuwaunganisha diaspora wote  wa Kitanzania ktk taasisi moja ili kupata taarifa mbalimbali zinazowahusu diaspora wa Tanzania kwa haraka na kushauriana kuhusu mahitaji ya diaspora na jinsi ya kuyatetea.  Kupata taarifa hizo bonyeza Link hii 


Kujiunga na Baraza bonyeza link hii http://www.tdcglobal.org/member-register/

Karibu sana

NB:Ukipatwa na tatizo lolote kwenye kujiunga piga simu
+47 46 21 86 09

Ukipata taarifa hii mjulishe na mwenzako.

Agnes Lerdorf 
Kamati ya Mahusiano na Umma

Tanzania Global Diaspora Council
Pamoja Tunaweza - Mtu Kwao Ndio Ngao
Wednesday, March 21, 2018

Kutoka ubalozini Stockholm kuhusu vitambulisho vya taifa na pasipoti mpya

Kwa Viongozi wa Jumuiya ya Watanzania,

Ubalozi umepokea taarifa toka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
(NIDA) kuhusu usajili wa Watanzania waishio nje ya nchi (Diaspora).


Mamlaka imemteua Bi.Rose Mdami (Simu ya mkononi namba +255 713 412 871) kuwa afisa dawati atakayeshughulikia masuala ya diaspora ndani ya mamlaka ya NIDA. 

Dawati hili litatoa huduma kwa haraka kwa diaspora katika jengo la magereza lililopo katika barabara ya Kivukoni mjini Dar es Salaam.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na Bi. Mdami simu ya mkononi namba 

+255 713 412 871

Kwa taarifa zaidi tembelea tovuti ya NIDA 

http://nida.go.tz/swahili/index.php/kitambulisho-cha-taifa


Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa   http://nida.go.tz/swahili

Tafadhali wafahamisheni wanachama wa jumuiya zenu. Kuwa na kitambulisho cha Taifa kitasaidia pia katika zoezi la kuomba pasipoti mpya. Kwa hiyo ni muhimu kwa Watanzania kujitahidi kuomba vitambulisho wanapokuwa wamekwenda likizo Tanzania.


MATIKU KIMENYA
UBALOZI WA TANZANIA
KWENYE NCHI ZA NORDIC
NA ZA BALTIC
STOCKHOLM.
SWEDEN
http://www.tanemb.se
Sunday, February 18, 2018YAHUSU UTARATIBU WA MAOMBI YA PASIPOTI MPYA YA KIELETRONIKI YA TANZANIA KWA WAOMBAJI WA NDANI NA NJE YA TANZANIAUbalozi wa Tanzania Sweden umepokea maelezo toka Wizara ya Mambo ya Ndani, Idara ya Uhamiaji juu ya utaratibu wa maombi ya pasipoti mpya kama ifuatavyo:

"Idara ya Uhamiaji imeanza kutoa Pasipoti mpya za kielektroniki kwa Watanzania kuanzia tarehe 31. Januari 2018. 

Pasipoti za zamani zitaendelea kuwa halali kwa matumizi hadi ifikapo tarehe 31.Januari 2020. 

Utaratibu mpya wa maombi kwa sasa utawahusu waombaji wa pasipoti waliopo ndani ya nchi tu. 

Kwa waombaji waliopo nje ya nchi wataendelea na utaratibu wa zamani na kupewa pasipoti za zamani mpaka hapo mitambo ya kuchukua alama za vidole itakaposimikwa kwenye balozi zetu". 

Hivyo kwa taarifa hii watanzania mnaoishi nchi za Nordic na Baltic mtaendelea kutumia pasi mlizonazo na mkiomba mpya mtapata kama hizi za zamani mpaka hapo ubalozi utakapowezeshwa kupokea maombi ya pasi mpya.

Ukipata taarifa hii mwambie na mwingine!

MATIKU KIMENYA, 
KAIMU BALOZI 
UBALOZI WA TANZANIA 
NCHI ZA NORDIC NA 
ZA BALTIC, 
STOCKHOLM
SWEDEN.


Saturday, August 19, 2017


Tunasikitika kutangaza kifo cha Sadiki Rajabu Bulibha, kilichotokea Oslo, Norway Jumatano, 16. Agosti 2017Mwili wa marehemu uko hospitali kwa uchunguzi utakaofanyika kati ya Jumatatu na Jumatano wiki ijayo. 

Chama Cha Watanzania Oslo kitawataarifu mipango ya mazishi wiki ijayo.

Mwenyezi Mungu Amlaza Pema, Ameen!


Tuesday, February 28, 2017

Mazishi ya Marehemu Abdallah Khelef Shauri "Dullah" Nchini Norway jana Jumatatu 27.Februari 2017


Sofia Abdallah Khelef Shauri (mtoto wa marehemu Abdallah  Khelef  Shauri) akiweka shada la maua la uchungu katika kaburi la baba yake baada ya kuzikwa jana.


Familia ya Shauri Mjaka na ndugu zake inatowa shukrani kwa Wananchi Wote walioshiriki kwa njia moja kuungana na familia hiyo katika kipindi chote cha msiba wa mtoto wao Abdallah Khefel Shauri «Dullah» katika kipindi kigumu cha msima huo uliotokea nchini Norway siku ya Jumamosi iliopita na kufikia tamati ya kukamilisha shughuli za mazishi zilizofanyika jana nchini Norway katika majira ya mchana saa 6:00 kwa kuuhifadhi mwili wa marehemu kwa kukamilisha taratibu zote za mazishi, Skoger Drammen.

Tunatoa shukrani kwa mzazi mwenziwe Mama Sofia kwa mchango mkubwa aliotoa kufanikisha maziko hayo. Tunatoa shukrani za dhati kwa Mama Sofia Inshaallah Mwenyenzi Mungu atakujalia kila la kheri katika maisha yako. 

Pia na marafiki waliofika kutoka nchi jirani na kuwahi msiba huo kumshindikia
mpendwa rafiki yao. 

Inatowa shukrani kwa Jumuiya zote za Watanzania wanaoishi nje kwa umoja wao kwa hali na mali kuweza kufanikisha suala hii kwa ushirikiano wao. Tunatoa shukrani kwa uongozi wa Jumuiya watanzania Wanaoishi nchini Norway kusimamia suala hili hadi mwisho kufanya taratibu za mazishi ya Ndugu yetu. Tunatoa Shukrani kwa Jumuiya ya Kiislamu ya Watanzania Norway na Ndugu Hassan na Jamal kusimamia hadi kukamilika.

Hatuna cha kuwalipa kwa hili inshalla Mwenyenzi Mungu atawajalia kila la kheri na moyo wa imana kwa hili na lengine.

Ameen.