Friday, July 20, 2007

Jaji Mkuu Mpya wa Tanzania, Brigedia Jenerali Agostino Ramadhani

Rais Jakaya Kikwete jana amemwapisha Jaji Agostino Ramadhani kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania, baada ya Jaji Mkuu Barnabas Samatta kustaafu rasmi. Jaji Ramadhan amewahi kuwa Jai katika mahakama ya Afrika Mashariki ambako alikuwa yeye na Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, Jaji Joseph Warioba. Sambamba na kuwa mwanasheria na mwanajeshi, Jaji Ramadhan pia ni mpiga kinanda maarufu katika kwaya ya Kanisa la Anglikana jijini Dar es Salaam.

No comments: