Friday, August 31, 2007

Sabina Mzuanda, Mbongo anayebanana nao majuu....

Sabina Mzuanda a.k.a Eite Sabina Mzuanda Wilburn
__________________________________

Mbongo huyo mwenye ndoto za kuingia Hollywood, kimakazi yupo Marekani na ameshacheza katika filamu kadhaa na kushiriki katika vipindi kibao.....Ni Sabina Mzuanda.

Eita Sabina Mzuanda alizaliwa jijini Dar es Salaam na kupata elimu yake Kenya, Uingereza na Marekani

Eita ameolewa na mwanajeshi akitumia jina la Eite Sabina Mzuanda Wilburn na wanaishi Texas pamoja na mbwa wake wawili

Anasema alianza kuwa na interest sanaa masuala ya sanaa tangu alipokuwa shuleni ambako alikuwa akiigiza maigizo na aliweza kuwashika watu kwa jinsi alivyokuwa anauvaa uhusika katika nafasi tofauti tofauti.

Kutokana na juhudi zake za kujichanganya huku na huko katika miji tofauti huko Texas atlast amefanikiwa kupata wakala Sao Antonio inayojulikana kama Rome Talent Agency ....ambayo atakuwa anafanya nayo kazi ya kuigiza filamu

...Pamoja na majukumu ya kazi yangu ya kutwa bado najitahidi niweze timiza ndoto zangu katika uigizaji na linalonisukuma zaidi ni ule moyo ambao wazazi wangu huwa wananipa kila siku kwa kunikumbusha nimtangulize mungu kwanza na kuniambia nijiamini na nisijali mtu yeyote atakaenivunja moyo...alisema Sabina

Akieleza alipoanzia Sabina anatanabaisha kwamba yeye anaamini muigizaji unatakiwa uanzie mahali na kwa yeye alianzia mbali kwa kujibidiisha na kujicommit kutimiza ndoto na matakwa yake....alianza kwa kufanya kazi ya ziada katika vipindi maarufu vya runinga ikiwemo Prison Break, Inspector Mom na Friday Night Lights.

Pia alipata nafasi ya kufanya kazi na filamu kama Grindhouse ambapo alicheza kama Zombie.Nyengine ni filamu ya Elvis and Annabelle ambako alicheza ka mhabarishaji (Bado haijaingia sokoni),Nyengine ni zile za ndani ya Texas kama I want to see my skirt and Technocracy ambayo inarusha mtandanoni na ilipata nafasi ya kushania tuzo ya Emmy .

Mbali na hizo pia ameshiriki katika filamu ya Gary
the Tennis Coach kama flight attendant ambayo iliigizwa Texas miezi iliyopita,

Kwasasa Sabina anaigiza katika filamu inayoenda kwa jina la Murmur ambayo ameigiza kama Afrivan Voodoo Priestess.

Mbali na kuigiza Sabina anapendelea kujichanganya na jamii ambapo kwa sasa ni mwanachama waReel Women Organization, San Antonio Actors network, Austin Film Society na Texas Motion Picture Allience

Mwezi wa sita mwaka huu akiwa na chama cha Reel Women alijitolea kufanya kazi kwa siku 2 na aligundua kwa....ni vizuri kwani ilimkutanisha na watu tofauti tofauti ambayo wengi wana interest sawa nae ambao wanako radhi kujifunza either wakiwa kwenye camera

Kila la kheri Sabina

Kutoka: http://www.darhotwire.com/maisha/news/2007/
08/31/mbongo__anayebanana_nao_majuu.html



No comments: