Saturday, September 22, 2007

Jimama ladatishwa na Dully Sykes

Dully Sykes "Misifa"


Chanzo cha Ijumaa, kiliwapasha waandishi wetu kuwa Kuruthumu ni mkazi wa Mombasa, Kenya na ametua Tanzania wiki mbili zilizopita kwa lengo la kumnasa Dully Sykes a.k.a Mr. Misifa.

Chanzo hicho ambacho ni ndugu na mwanamuziki huyo, kiliongeza kwamba jimama hilo la Mombasa, limeahidi donge nono la milioni moja kwa mtu ambaye atafanikisha kwa haraka zoezi hilo.

"Ni mwanamke mtu mzima, anaweza kuwa na umri wa kati ya miaka 33 na 35, mimi ndiye alinifuata na kuomba nimuunganishe na Dully, akaniambia nikiweza atanipa milioni moja au mtu yeyote akimsaidia basi atampa kiasi hicho cha pesa.

"Aliniambia yeye ni mjane, mume wake ameshafariki, amemuachia mali nyingi, kwahiyo hivi sasa anatafuta mtu wa kumliwaza," kilisema chanzo hicho na kuongeza: "Anasema Dully ndiye chaguo lake na akikubali ataondoka naye kwenda nyumbani kwake Mombasa.

"Mimi nimefikiria vitu vingi, pengine huyo mama anaweza kuwa na ukimwi, kwahiyo tamaa yangu ya hela ikamponza ndugu yangu, alinipa na picha nimuoneshe Dully, lakini mimi sijamuonesha wala kumwambia jambo lolote," kilieleza chanzo hicho.

Wiki iliyopita, gazeti hili lilimzuga Kuruthumu kwamba lipo pamoja na Dully katika Eneo la Sinza, Dar es Salaam ambapo mwanamke huyo alifika mara moja.

Hata hivyo, baada ya kujua amedanganywa, Kuruthumu alikuwa mkali, lakini alipotambua kuwa waliomdanganya ni waandishi wa habari, akanywea kama maji ya mtungini.

Aidha, Kuruthumu alikiri kwamba anamtafuta Dully Sykes, ingawa alipata kigugumizi alipoulizwa kama ni kwa sababu za kimapenzi.

"Siyo lazima niwaambie namtafuta kwa shughuli gani, lakini nina shida naye, huyo aliyewaambia kwamba nitampa milioni moja mtu atakayenisaidia ni mzushi," alisema Kuruthumu na kuongeza kwamba huwa anawasiliana na Dully Sykes kwa simu ya mkononi.

Akiongea na gazeti hili, Dully Sykes alisema, hashangai mwanamke huyo kumtaka kimapenzi, kwani amekuwa akipigiwa simu za kumtongoza kwa wastani wa wanawake 25 kwa siku.

"Hivi huyo mwanamke ana hela eeh, vipi ni mzuri eeh? Lakini mimi 'simaindi' mambo hayo, nina mchumba wangu," alisema mwanamuziki huyo na kuongeza kuwa hajui kama miongoni mwa wanawake 25 ambao humtongoza kwa siku na Kuruthumu yumo.

Chanzo cha habari Global Publisher Tanzania.

No comments: