Thursday, September 20, 2007

Mfahamu: Khadija Mwanamboka, mbunifu wa mitindo/mavazi

Khadija akiwa na mtoto Hussein.Picha na Esther Mngodo.

Ingawa dhana ya “ubunifu wa mitindo” bado haijatapakaa sana nchini Tanzania,wapo wabunifu wa mitindo ambao kila kukicha wanazidi kuitambulisha sanaa hii kwa watanzania walio wengi kwa namna mbalimbali. Mmojawapo ya wabunifu hao wa mitindo ni Khadija Saad Mwanamboka. Akiwa na umri wa miaka 30 tu ameshajijengea jina miongoni mwa wabunifu wa mitindo nchini Tanzania.
Khadija haishii kwenye kutengeneza viwalo tu bali ni mmojawapo wa wale celebrities ambao wanaikumbuka jamii yao na hivyo kila mara kukuna vichwa ni jinsi gani wanaweza kusaidia kila inapowezekana. Hivi karibuni ameanzisha asasi isiyo ya kiserikali (NGO) inayoitwa TANZANIA MITINDO HOUSE. Asasi hiyo inalenga mambo makuu mawili; kwanza kuwasaidia wabunifu wa mitindo wenzake na pia wale chipukizi katika kutimiza ndoto zao za mahiri zaidi na hivyo kuzidi kuitangaza mitindo ya kutoka Tanzania duniani kote. Khadija anasema wapo watu wengi tu wanaotamani kuwa wabunifu wa mitindo lakini hawajui wafanyeje wala waanzie wapi. Anawakaribisha kuwasiliana naye.
Pili asasi hiyo inalenga katika kusaidia watoto yatima, walioathirika na ugonjwa wa Ukimwi na wale wasiojiweza aidha kutokana na umasikini au sababu nyinginezo. Kauli mbiu ya kampeni yake ameiita “Tanzanian Designs For Lives”.
Lakini Khadija mwenyewe ametokea wapi? Alianza vipi kazi zake za ubunifu wa mitindo? Ana ushauri gani kwa vijana wenzake? Ana ujumbe gani kwa watanzania kuhusiana na suala la mitindo ya kitanzania? Kwa hayo na mengi mengineyo BongoCelebrity tumefanya naye mahojiano yafuatayo; (Kutoka Bongo Celebrity)

No comments: