Naam! Wanakijiji wenzangu, picha zinajieleza zenyewe. Bado nina picha nyingi, hata hivyo, naona hizi zinatosha kwa sasa. Ambazo hamkuziona zitabaki kwenye maktaba ya kijiji. Natumaini, hata kama hamkuwepo harusini, mmeweza kuwa pamoja na dada yetu DaMija kupitia picha hizi. Hakika, ilikuwa ni shughuli ya mwanablogu mwenzetu, mwanakijiji mwenzetu, hivyo basi, ni shughuli ya kijiji. Na ndio maana ya kupewa upendeleo huu usio wa kawaida hapa kijijini kwetu. Kwa mara nyingine tena, kwa niaba ya wanakijiji wote, tunawatakia DaMija na mwenza wake katika maisha, shemeji David Manju, kila la kheri katika maisha yao ya ndoa. Asanteni!
Asante Ndg. Maggid Mjengwa kwa picha nzuri. Kweli ilikuwa harusi ya aina ya pekee!!!
http://mjengwa.blogspot.com/
No comments:
Post a Comment