Saturday, October 20, 2007

Makocha hao ambao walitua jana katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere majira ya saa 3:30 asubuhi kwa kutumia ndege ya Shirika la Ndege la Kenya (KQ) ni Kocha Mkuu, Spaso Solouski na msaidizi wake, Kondic Dusan.

(Blogu ya wapenzi wa Yanga)

Ingawa Manji hakupatikana jana kuzungumzia ujio wa makocha hao, habari kutoka chanzo chetu kilichopo ndani ya klabu hiyo zilidai kuwa, mfadhili huyo amewaleta baada ya kumkataa Kocha Mpoland, Wojciech Lazarek ambaye alidai kuwa ni mzee.

Kiliendela kutueleza kuwa, kama makubaliano yatafikiwa mapema, watajaribiwa katika mechi dhidi ya watani wao wa jadi Simba, inayotarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja mpya wa Taifa jijini Dar es Salaam, Octoba 24, mwaka huu.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Yanga, Imani Madega aliliambia gazeti hili kwamba, makocha hao watakaa nchini kwa muda wa wiki mbili, ambapo watautumia muda huo kuingalia timu ya Yanga.

“Makocha wetu waliokuja leo (jana) wanatarajia kwenda moja kwa moja Morogoro kwa ajili ya kuingalia Yanga, katika baadhi ya mechi zake za Ligi Kuu ya Tanzania Bara inayoendelea hapa nchini, wakati huo tutaenelea kufanya nao mazungumzo,” alisema Madega.

Makocha hao wamekuja kwa ajili ya kuziba pengo lililoachwa na Mserbia, Milutin Sredojevic ‘Micho’ ambaye aliikacha timu hiyo hivi karibuni.

Baadhi ya Wanachama waliokuwepo uwanjani hapo, walifurahia ujio wa makocha hao na kudai kwamba klabu yao haina tofauti na zile za Ulaya.

“Sasa Yanga itakuwa tishio, wachezaji wazuri tunao, na makocha wazuri ndio hao, nasema hawatatukamata katika ligi na hata michuano ya kimataifa,” alisema Said Motisha, mwanachama wa Yanga.

Kwa sasa Yanga iko chini ya Kocha Mkuu wa muda, Mmalawi Jack Chamangwana akisaidiwa na Mwalimu wa makipa, Mkenya Razak Siwa.

Awali Manji alitishia kujitoa kuifadhili Yanga kutokana na kutofautiana na Madega, lakini hata hivyo, tofauti zao zilimalizwa na kukubaliana kuimarisha umoja na mshikamano klabuni hapo.

Wakati huo huo, habari zilizolifikia gazeti hili muda mfupi kabla halijakwenda mitamboni kutoka katika chanzo chetu kilichopo ndani ya kambi ya Yanga zinadai wachezaji wameahidiwa kumwagiwa mamilioni endapo wataifunga Simba.

Kutoka Global Publisherstz.com

No comments: