Monday, October 15, 2007



Mwanamke wa kwanza kuwa Meja Jenerali nchini Tanzania.
Pichani alipokuwa Brigedia Jenerali.


Rais Kikwete awapandisha vyeo wanajeshi 19


na Agnes Yamo

RAIS Jakaya Kikwete amewapandisha vyeo maofisa wanne wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kuwa mameja jenerali na wengine 15 kuwa brigedia jenerali kuanzia Oktoba 8, mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Idara ya Uhusiano ya Makao Makuu ya Jeshi, miongoni mwa maofisa waliopandishwa vyeo ni pamoja na wanawake watatu.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa hii ni mara ya kwanza katika historia ya JWTZ kwa maofisa wake wa kike kupanda hadi kufikia ngazi ya meja jenerali, tagu jeshi hilo lilipoanzishwa 1964.

“Hii ni mara ya pili kwa mwanamke kupandishwa cheo kutoka cheo cha Kanali na kuwa Brigedia Jenerali,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Inawataja waliopandishwa kutoka brigedia jenerali kuwa meja jenerali kuwa ni Zawadi Madawili, Alfred Mbowe, ambaye ni msemaji wa jeshi hilo, Servas Hinda na Wynjones Kisamba.

Waliopandishwa kutoka kanali kuwa brigedia jenerali ni Kelvin Msemwa, Albert Kigadye, Sebastina Chiwangu, Patrick Mlowezi, Daniel Igoti, Salum Kijuu, Farrah Mohamed na Gerald Kiswaga.

Wengine ni Julius Mbilinyi, Mabula Mashauri, Vincent Mritaba, Charles Jitenga, Charles Muzanila, Grace Mwakipunda na Lilian Kingazi.

Kutoka Tanzania Daima.

No comments: