* Wapo manaibu watano wa bara
* Pia wamo mawaziri watatu wa SMZ
* Waandishi wa habari nao hoi
Na Waandishi Wetu Dar , Dodoma
MATOKEO ya uchaguzi wa nviongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) yameonyesha sura tofauti na matarajio ya wengi hasa kwa baadhi ya wagombea wenye majina makubwa kujikuta wakitupwa nje bila matarajio yao.
Manaibu waziri watano ni miongoni waliokosa nafasi katika uwakilishi wa Viti 20 NEC nao ni pamoja na Naibu waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Dk David Mathayo, Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mshariki Dk Deodorus Kamala na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja.
Wengine ni Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mwantumu Mahiza na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi Ritha Mlaki aliyegombea nafasi hiyo kupitia kundi la wanawake.
Pia wapo manaibu waziri watatu wa SMZ wametupwa chini ambao ni Jabir Makame Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo, Khatib Suleiman ambaye ni Naibu Waziri Kilimo, Mifugo na Mazingira na Dk Mwinyi Haji Makame, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais.
Katika nafasi za kundi la wanawake Tanzania Bara kuna Mbunge wa zamani wa Afrika Mashariki na sasa Mbunge Beatrice Shelukindo. Pia yupo Mbunge Tatu Ntimizi na Katibu Mkuu mstaaf wa UWT Halima Mamuya.
Kwenye kundi la Vijana kuna wagombea Hussein Mohamed ambaye alionekana kufanya kampeni maeneo mengi ya nchi na kuonyesha kuwa angeibuka mshindi naKiongozi katika ofisi ya UVCCM taifa, Fransis Issack walitupwa.
Kwa upande wa Issack, hili ni pigo lingine kufuatia kupoteza nafasi zote alizogombea mkoani Singida huku akitajwa kuwa na nia ya kusaka kiti cha Mwenyekiti wa UVCCM ngazi ya taifa katika uchaguzi utakaofanyika mwakani.
Wengine katika kundi hilo ni Vanessa Mugeta ambaye naye alifanya kampeni kubwa na kuonekana kuweza kushinda. Pia wapo viongozi wa UVCCM katika ngazi za mkoa kama Jasinta Mboneko na Sixtus Mapunda ambao wote wamedondoka huku wakielezwa kuwa walitarajia matokeo mazuri ili kuendeleza nia ya kusaka madaraka ya juu katika jumuiya hiyo.
Katika kundi la wazazi Tanzania Bara, hapa kulikuwa na wagombea wengi ambao ni wabunge. Katika kundi hili kuna jina moja tu la aliyeshinda ambaye si mbunge ambaye ni Nondo Mohamed.
Lakini pia Danhi Makanga, Ruth Msafiri, Thomas Ngawaiya
na Tambwe Hiza wamepoteza katika kundi hili. Ngawaiya na Hiza
walitoka upinzani na walitarajiwa kupewa kura za huruma jambo ambalo halikufanyika.
Wengine nni pamoja na wabunge Margareth Agness Mkanga, Zuhura Mikidadi na mhamasishaji wa tenzi wa CCM, Salim Shomvi Tambalizeni, Naibu Meya wa Ilala Mustafa Yakub, Mkuu wa Mkoa wa Mara Isdore Shirima na Mkuu wa Wilaya ya
Frank Uhaula walikosa nafasi hizo.
Wanasiasa wengine maarufu waliokosa nafasi baada ya kupata kura chache ni Wilson Masilingi, Brigedia Jenerali Mstaafu Hassan Ngwilizi, Tarimba Abbas, Filbert Bayi, Enock Chambiri, Christopher Gachuma, Charles Kagonji, Lukas Kisasa, Pascal Mabiti, Dk James Msekela, Profesa Idrisa Mtulia, Abeid Mwinyimsa na Job Ndugai.
Wengine ni wandishi wa habari Jacqueline Liana, Jeni Mihanji na Novatus Makunga.
Katika kundi la viti 20 kutoka Zanzibar, hapa kumekuwepo na maswali kiasi kuhusu namna kura zilivyojipanga.
Wengine waliokosa ni Shyrose Banji aliyekuwa miongoni mwa wagombea watatu wa kike katika kundi hili.
Katika kundi hili namna kura zilivyojipanga ni sawa na kilichotokeakatika uchaguzi wa CCM mwaka 2002 ambapo matokeo yamekuwa yakifuata nafasi za madaraka.
Sababu ya kuwepo kura za aina hii inaelezwa kuwa ni kutokana na kuwepo baadhi ya wanaojiandaa kwa ajili ya nafasi za kisiasa siku za usoni na pia kuwawekea mazingira mazuri viongozi wa serikali na chama ili kuonyesha wanakubalika na wanachama wote.
Hata hivyo, uchaguzi huo ulifanyika katika hali ya utulivu na amani na hata matokeo yaliposomwa wajumbe na wagombea wote waliyapokea bila kinyongo.
Katika nafasi mbalimbali zilizokuwa zinawaniwa, eneo lililokuwa gumu zaidi ni la viti 20 kwa Tanzania Bara na Visiwani huku ikionekana wazi kuwa, kuna watu waliokuwa wamejiandaa kupata kura nyingi na kuhakikisha kuwa wenzao hawafurukuti.
Kwa upande wa Zanzibar, uchaguzi huo ulionyesha jinsi kambi za kuwania urais mwaka 2010 zitakavyokuwa. Kwa hiyo utata utabakia kama wajumbe wa CCM Bara watabakia na nguvu ya kuwachjagulia wenzano wa Zanzibar mgombea urais bila kuangalia kukubalika kwake na Wazanzibari.
Matokeo ya uchaguzi huo kufuatana na makubdi yalikuwa: Kundi la Wanawake Bara walioshinda na kura zao kwenye mabano ni Margaret Sitta (1780),Zakia Meghji (1207), Pindi Chana (1203), Anne Makinda (1146), Diana Mkumbo Chilolo(1103), Anna Malecela (993), Dk Rehema Nchimbi (887), Shamsa Mwangunga (850), Khadija Kopa (842), Asha Baraka (769), Kate Kamba (706) na Sofia Simba(686).
Kundi wanawake kwa upande wa Zanzibar ni Mwaniju Abdalla (1,151), Fatma said Alli (1082) Yasmin Aloo (1,064), Amina Mabrook (1,030) Catherine Lao (1,064) na Aisha Bakari Makame (943).
Kundi la Vijana Bara ni Zainab Kawawa (1390), Violet Mzindakaya (1165), Nape Nnauye (1056), Jerry Slaa (994), Sarah Ally (935), Suleiman Chambi (862), Beno Malisa (857), Edwin Sanga (804), Lucy Mayenga (770).
Vijana Zanzibar ni Hawa Sukwa Said (980), Hamad Yusuph (894), Hadila Hilal (886), Michael Bundala (845), Ashura Ismail (808), Suleiman Muhsin Haji (770).
Kundi Jumuia ya Wazazi Bara ni Stella Manyanya aliongoza kundi hilo kwa kura 948, akifuatiwa na Dk Zainab Gama (818) Mussa Zungu (730) Adam Malima (698) Mohammed Nondo (670 ) na Richard Nyaulawa (669) walishinda kuwakilisha kundi hilo.
Wazazi Zanzibar walioshinda ni Dogo Iddi Mabrouk, hassan Rajab, Fatma Haji(736), Mtumwa Yusuph Beya (715).
Wazazi Zanzibar; Oogo Iddi Mabrouk, Fatma Abeid Haj, Mtumwa Yussuf Peya, Hassan Rajab Khatib.
Kundi la viti 20 Zanzibar; Katika kundi hili linaonyesha kuwepo kura za itifaki au nafasi ya nguvu za wajumbe wa Bara katika kuwapa kura wagombea wa Zanzibar wanaowafahamu.
Aliyeongoza ni Makamu wa Rais Mohamed Shein kwa kupata kura 1663, akifuatiwa na Waziri Kiongozi wa Zanzibar Shamsi Vuai Nahodha (1525), Dk Hussein Mwinyi ambaye ni Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muuungano (1496) kisha Waziri Kiongozi Mstaafu Dk Gharib Bilal (1366).
Matokeo haya ni wazi yanatoa picha ya namna nafasi ya urais wa Zanzibar kwa mwaka 2010 itakavyokuwa. Bilal ana nguvu na mtaji mkubwa wa wanachama Zanzibar tofauti na Shein, Mwinyi na Vuai Nahodha. Kama hali itakuwa hivi ni wazi kuwa nguvu ya Bara itaweka tena rais mwingine wa Zanzibar kama
ilivyokuwa kwa Karume mwaka 2000.
Wengine katika kundi hilo ni; Salehe Ramadhan Ferouz (1352), Mohamed Seif Khatib (1346), Samia Suluhu Hassan (1281), Salum Msabah Mbarouk (1151), Khadija Hassan Aboud (1076), Mansoor Yusuf Himid (1073), Omar Yusuf Mzee (1022), Balozi Seif Alli Idd (997), Moh’d Hassan Moyo (959), Profesa Makame Mnyaa Mbarawa (958), Maudlin Cyrus Castico (950), Vuai Ali Vuai (943), Brigedia Adam Mwakanjuki (936), Thuwaybah Edington Kissasi (860) na mwisho ni Abdalla Sharia Ameir.
Katika nafasi Vijana Tanzania Bara walioshinda ni; Lucy Mayenga aliyepata kura 770, Edwin Mgante (804), Beno Malissa (857), Suleiman Masoud (862) Sara Msafiri (935), Jerry Silaa (994), Nape Nnauye (1056), Violet Mzindakaya (1165), Zainab Kawawa (1390).
Kundi la wazazi Tanzaia Bara; Richard Nyaulawa alishinda kwa kupata kura 669, Mohamed Nondo (679), Adam Malima (698), Mussa Zungu (730), Dk Zainab Gama (818) na Stella Manyanya (948).
Katika kundi la Viti 20 vya Itifaki kwa upande wa waliochaguliwa ni Waziri Mkuu Edward Lowassa aliweza kuibuka mshindi akiongoza kwa kura 1,681, akifuatiwa na Waziri wa Miundombinu Andrew Chenge aliyepata kura 1,530.
Wengine ni Katibu mkuu wa CCM Yusuph Makamba(1,510), Waziri waMambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (1,281), Naibu Katibu Mkuu CCM Jaka Mwambi (1,239), Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Profesa Juma Kapuya (1,216).
Katika Kundi hilo wengine ni mwanasiasa wa siku nyingi Abdulrahman Kinana (1,204) Christopher Gachuma (1,181) Waziri wa Kilimo na Chakula Stephen Wassira (1,107) Katibu Mwenezi wa CCM Aggrey Mwanri (1,068) Naibu Waziri wa Miundombinu Makongoro, Mahanga (1067) na Waziri Mkuu wa zamani Frederick Sumaye (1065).
Weingine ni Mbunge John Komba (1056), Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Siasa na Uhusiano wa Jamii), Kingunge Ngombale Mwiru (1023), Mkuu wa Mkoa wa Dodoma William Lukuvi (943), Waziri wa Kazi Ajira na Maendeleo ya Vijana, Kapteni John Chiligati (910), Katibu Mkuu UVCCM, Amos Makala (871), Profesa Samwel Wangwe (817), Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Profesa David Mwakyusa (754) na Jackson Msome (747)
Kwa upande wa Zanzibar waliochaguliwa ni Makamu wa Rais, Dk Alli Mohamed Shein aliongoza kundi hilo kwa kupata kura (1965) akifuatiwa na Waziri Mkuu Kiongozi Shamsi Vuai Nahonda (1525), Dk Hussein Mwinyi (1496) Dk Gharib Bilali (1366) Ramadhani Ferouz (1352), Salum Msabaha (1151), Yusuph Kimiti, Mzee Omari (1,022), Balozi Alli Iddi (987) Moyo Mahmoud (959) Dk Mbarawa, Muhsin Kastiko (950), Vuai Alli Vuai (943), Brigedia mstaafu Mwakanjuki (936) na Waiba Kisasi (860).
Kwa upande wa nafasi ya Mwenyekiti, Jakaya Kikwete akichaguliwa tena kwa kura 1887 na kukataliwa kwa kura tano na nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bara, Pius Msekwa alipata kura1875 na akikataliwa kwa kura nne na Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Abeid Karume alipata kura 1886 na kura moja ya hapana.
Kutoka gazeti mtandaoni la Mwananchi, Jumatatu 5. Novemba 2007
No comments:
Post a Comment