Saturday, November 03, 2007

yastopishwa!

Katika hatua ambayo huenda ikawa ni mara ya kwanza kutokea ktk muziki wa Bongo Flava,video mpya ya wimbo ‘Simama tucheze’ ya msanii Aboubakar Katwila 'Q- Chilla' imepigwa marufuku kuoneshwa kwenye vituo kadhaa...kwa maelezo kuwa ndani yake kuna vitendo vingi visivyoendana na maadili ya kitanzania.

Video hiyo iliyorekodiwa Mombasa,Kenya...inadaiwa kuwa imekuwa ikionesha vitendo vya Ngongo..vilivyoonekana kuvikera vituo hivyo.

Mmoja wa watangazaji wa kituo kimoja maarufu jijini alikaririwa akisema...."Ni vigumu kwa video hiyo kuoneshwa kwenye kituo chochote kwani imejaa vitendo vya ngono na haikuzingatia maadili ya kitanzania kabisa."

Akiongea hivi karibuni,Q-Chilla ...alisema hana taarifa yoyote ya kupigwa marufuku kwa video yake na kueleza kuwa anachojua yeye kuna baadhi tu ya vituo ambavyo vimegoma kuipiga....huku akiuliza kwa mshangao ni kwanini
video kibao za Marekani watu wanafanya mambo machafu kibao na bado zimekuwa zikioneshwa kila kukicha?

Akiendelea alisema hata kama video yake itazuiwa kuoneshwa nchini, bado ana uhakika itaoneshwa nje ya nchi alikoisambaza na anaamini itamtambulisha vyema katika soko la kimataifa la muziki.

Kutoka DarHotWire.

No comments: