Thursday, December 20, 2007

Flaviana Matata ndani ya France..

Picha za juu ni latest kutoka France zikimuonyesha mrembo
Flavian Matata akiwa kwenye photoshoot mbalimbali juzi nchini humo.

Tovuti ya Global beauties ambayo ni mashuhuri kwa kutoa habari na tathmini ya mashindano mbalimbali duniani kote imetoa warembo 36 bora wanaowania kuwa Mwanamke mwenye mvuto zaidi duniani (Sexiest Woman alive) kwa kuwaunganisha washindani wa mashindano 5 makubwa ya kimataifa na kuwachuja.


Hivi sasa tathmini ya awali imeonyesha kutoka bara la Afrika warembo wafuatao:


Mrembo wa Angola katika Miss Universe na MissWorld –Micaela Reis, Flaviana Matata wa Tanzania aliyetuwakilisha katika mashindano ya Miss Universe, Bokang - Miss South Africa kutoka Mashindano ya Miss Earth.


Flaviana aliyeibuka mshindi wa 6 katika mashindano ya Miss Universe mwaka huu nchini Mexico aliweza kuweka historia kwa kuwakilisha nchi yetu kwa mara ya kwanza katika mashindano haya makubwa kupita yote duniani, na kufanya vizuri.


Flaviana ambaye hivi sasa yuko nchini Ufaransa kwa photoshot alieleza kwa njia ya simu furaha yake kuingia 35 bora akisema kuwa kwa njia hii anaendelea kutangaza nchi yake. 12 bora na mshindi watapatikana kupitia kura za washabiki mbalimbali.


Mkurugenzi wa kitaifa wa Miss Universe Tanzania, Maria Sarungi Tsehai aliwaomba watanzania wote ndani na nje ya nchi wampigie kura Flaviana kupitia tovuti ya
www.globalbeauties.com

Kutoka: http://haki-hakingowi.blogspot.com/



No comments: