Monday, January 28, 2008

Africa Cup of Nations 2008

Kundi A


The Black Stars 2


The Atlas Lions 0


Wenyeji wa fainali za mataifa ya Afrika, The Black Stars (Nyota nyeusi) wamefanikiwa kuingia kwenye robo fainali baada ya kuwafunga Simba wa milima ya Atlas (Morocco) kwa magoli 2 - 0.
Magoli yote mawili yalipatikana kwenye kipindi cha kwanza. yalikuwa ni matokeo ya ushirikianomzuri kati ya Michael Essien na Sulley Muntari. Goli la kwanza lilipatikana dakika ya 26, baada ya Muntari kupiga frikiki safi iliyowapita wachezaji wa Morocco walioweka ukuta kulinda goli lao na kumfikia Essien aliyefunga kirahisi. Goli la pili lilifungwa na Muntari baada ya kupokea pasi murua toka kwa Essien.


Mashabiki wa The Black Stars wakiishangilia timu yao.

The Black Stars wakishangilia goli la kwanza lililofungwa na Essien (namb. 8)



Syli Nationale 1

Brave Warriors 1


Guinea (Syli Nationale) wamefanikiwa kuingia robo fainali kwenye kundi hili. Guinea walifungua mlango kwenye dakika ya 62 kwa goli lililofungwa na Souleymane Youla. Goli la kusawazisha la Mashujaa Werevu (Namibia) lilifungwa kwenye dakika ya 81 na Brendell.


Mfungaji wa goli la Guinea, Souleymane Youla.


Brian Brendell wa Namibia akishangilia goli la kusawazisha.


Ghana wameingia robo fainali wakiwa na pointi 9, Guinea pointi 4, Morocco 1 na Namibia 0.



3 comments:

Anonymous said...

Mnaonaje mkitimia majina ya nchi kama Cameroun, Nigeria etc badala ya Lions na Eagles? Wengine twapata shida kujua kibwagizo kipi kina wakilisha nchi gani. Vibwagizo hivyo vitumike ndani ya habari instead. Tuwe proud na majina ya nchi zetu za Africa hata kama sisi TZ hatumo

Chama Cha Watanzania Oslo - CCW Oslo said...

Mdau tumekusikia. Asante kwa maelezo yako.

Mhariri wa blogu

Anonymous said...

Sasa ni Baab Kubwa, Ahsanteni CCW!