Wednesday, January 16, 2008

Jakaya Kikwete ziarani Bukoba.


jk akisalimiana na watoto yatima katika kituo cha watoto yatima katika kijiji cha Bwoki, wilaya mpya ya Misenyi, mkoani Kagera muda, mfupi baada ya jk kuzindua kituo hicho leo. Kituo hicho kimejengwa na Bi Anneke Luyt raia wa Uholanzi akisaidiana na Bwana Phillippe Krynen na marafiki zao.



jk akimpongeza Sheikh Mustapha Khalid Swidia, mkuu wa Madrasati Phalahi iliyopo Katoro, wilaya ya Bukoba vijijini, muda mfupi baada ya jk s kufungua madarasa mapya yatakayotumika kama sekondari mapya ya kiislam. Hafla ya uzinduzi huo ilifaynika katika eneo la Katoro .Rais Kikwete yupo mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi ya wiki moja kukagua maendeleo ya miradi mbalimbali na kufungua miradi mipya.



Baadhi ya Wanafunzi wa Kike wanaosoma katika sekondari mpya iliyopo chini ya Madrasati Phalahi Katoro wiklaya ya Bukoba vijijini waliohudhuria hafla ya ufunguzi uliofanywa na jk huko Katoro.

Picha na habari:
http://issamichuzi.blogspot.com/


No comments: