Sunday, January 13, 2008

Picha ya wiki toka Bongo Celebrity

Hizo ni nywele zake. Unaweza kumuita rasta ukipenda. Yeye mwenyewe sina uhakika kama anajiita rasta. Jamaa wengi waliofuga nywele za namna hii walikuwa ni wapiganaji wa Mau Mau nchini Kenya. Hapo jamaa alikuwa akionyesha nywele zake hivi karibuni huko Kenya baada ya kupiga kura yake. Alitoa ahadi kwamba endapo Raila Odinga angeshinda uchaguzi basi angezinyoa hizo nywele zake. Hilo halikutokea. Mumewe Lucy ameziokoa rasta hizi baada ya kufanya “muujiza” wa wazi wa uchaguzi. Bado tunaiombea Kenya iwe na amani. Hii ndio picha yetu ya wiki hii. Picha ya gazeti la The Standard la Kenya.


No comments: