“Chama Cha Wananchi (CUF) kimepokea na kutiwa moyo namaamuzi na hatua zilizoagizwa na Rais Jakaya MrishoKikwete za kukabiliana na ufisadi uliopindukia mipakakatika Benki Kuu ya Tanzania.Hatua hii imeleta matumaini kwa wananchi walio wengi kwa kuona kuwa Raisna Serikali ya Jamhuri ya Muungano imeanza kuchukuahatua madhubuti dhidi ya watumishi wa Serikali wanaojihusisha na hujuma kwa mali ya Watanzania.
Natoa pongezi za dhati kwa Mheshimiwa Rais JakayaKikwete kwa maamuzi mazito aliyoyachukua katikakipindi hiki ambacho wananchi walikuwa na shauku kubwakuona ni kwa uzito gain Rais angelilichukulia tatizo hili linaloelekea kuota mizizi nchini.
CUF inatoa wito kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU na Mwansheria Mkuu wa Serikali kukamilisha,katika kipindi kifupi iwezekanavyo, kazi waliyotumwa na Rais ya kutumia madaraka waliyokabidhiwa kufanya uchunguzi wa kina, nakisha kuwachukulia hatua za kisheria wahujumu wote wauchumi wa taifa letu bila ya woga, chuki walaupendeleo.
Aidha CUF inatoa wito kwa Rais kuendeleza kwa makini mapambano ya dhati dhidi ya wote waliojihusisha,wanaojihusisha nawatakaojihusisha na vitendo vya ainambali za hujuma dhidi ya rasilimali za nchi yetu nafedha za umma bila ya kujali vyeo vyao,umaarufu waona utukufu wao. Namhakikishia Rais kuwa mimi na CUF tutaendelea kumuunga mkono katika juhudi zake zakuokoa mali ya taifa letu na kusimamia maadili yauongozi na utumishi wa umma.
CUF pia inatoa pongezi maalum kwa Kambi ya UpinzaniBungeni chini ya uongozi mahiri wa Mheshimiwa HamadRashid Mohamed kwa ujasiri wao wa kuisaidia Serikali katika kufichua maovu yanayotendwa na wale waliokabidhiwa majukumu ya kuwatumikia Watanzania lakini badala yake wakajinufaisha binafsi bila yakuwaonea huruma raia masikini wa nchi hii.
Nimatumaini yangu kuwa Serikali itaendelea kushirikianana Kambi ya Upinzani katika kujenga enzi mpya ya siasaza kistaarabu na za mashirikiano zinazovuka mipaka yaitikadi kwa mambo yanayohusu maslahi ya taifa letu.
CUF inatoa wito kwa wananchi wote kuwa macho katikakulinda rasilimali za nchi yetu na kutoa taarifa kwamamlaka zinazohusika, wakiwemo wabunge, kwa zilehujuma ambazo wana ushahidi nazo.
CUF siku zote itashirikiana na Serikali, Bunge, nawatu wote wenye uzalendo na nia ya dhati ya kuisafishanchi yetu na uoza ambao kama utaachiwa uendelee utaliangamiza taifa letu.
DAR ES SALAAM
11 Januari, 2007
Directorate of Information and Policy Dissemination
The Civic United Front (CUF)
Party Headquarters
P.O. Box 3637
Zanzibar
Tanzania
Tel. (+)255 (0)747 414100 / (+)255 (0)741 257 665
E-mail: cufhabari@yahoo.com
Website: www.cuftz.org

No comments:
Post a Comment