Mji wa Zanzibar upo
Gizani kwa siku tano
MJI Zanzibar umefunikwa na giza zito kwa muda wa siku tano mfululizo kufuatia kukatika kwa umeme na hatimaye kusababisha biashara nyingi kusimama na nyingine kuharibika.
Akizungumza na mwandishi wa Mwananchi jana, Meneja wa Shirika la Umeme Zanzibar, Juma Isihaka Bakari alisema tatizo linatokana kuungua kwa nyanya za umeme zilizopita chini ya ardhi katika ya Mkele na Malindi hadi Mlandege.
Alisema mafundi wao wamefanya kazi tangu juzi usiku na mchana wakichimba maeneo hayo kutafuta hitilafu ilipo, lakini mpaka sasa hawafanikiwa.
Kutokana na hali hiyo maeneo mengi ya mji wa Zanzibar maduka makubwa yanayohitaji umeme kwa kiasi kikubwa yamefungwa
Katika baadhi ya maeneo yenye maduka ya samaki kama Darajani samaki wameoza na kuna harufu na kusababisha mazingira ya maeneo hayo kutokalika kutokana na harufu ya uvundo wa samaki.
Baadhi ya mahoteli ambayo hayana jenereta kama ya Bwawani ambayo ni ya serikali hakuna jenereta na hivyo baadhi ya wageni hotelini wameanza kuhamia mahali pengine kwenye unafuu.
Hospitali nyngi ya mjini hapa hazina jenereta hivyo kusababisha usumbufu mkubwa kwa wagonjwa, hususani ambao walitarajiwa kufanyiwa opasuaji.
Baadhi ya wafanyabiashara waliozungumza na mwandishi wa Mwananchi wameilalamikia hali hiyo na kulilaani Shirika la Umeme la Zanzibar kwa kuwaingiza katika hasara na kikubwa wakilalamikia kutokuwapo taarifa za uhakika.
Ibrahim Masudi ambaye ni mfanyabiashara wa duka kubwa Quality Super Market, alisema kwa sasa hapati wateja wengi kutokana joto na gizo hivyo kumfanya alifunga.
Mfanyabiashara mwingine wa samaki wa sokoni Zanzibar anayejishughulisha na uuzaji wa kamba na samaki wengine, Said Rashid alisema wamepata hasara kubwa kutokana na samaki kuoza.
"Yaani tunashangazwa sana na kitendo cha shirika la umeme kukata umeme, kwani kimetusababishia hasara kubwa," alisema Rashid.
No comments:
Post a Comment