Sunday, February 17, 2008

Ziara ya

George W. Bush Jr.

Tanzania

Rais George Bush akiteta na mwenyeji wake Rais jakaya Kikwete




Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete akimkaribisha Rais wa Marekani George Bush baada ya kutua uwanja wa kimataifa wa Mw Nyerere muda mfupu iliyopita..

Mke wa Rais Salma Kikwete akimkaribisha Rais Bush muda mfupi baada ya kuwasili uwanja wa kimataifa wa Mw Nyerere jijini Dar es Salaam jioni hii.

Rais Jakaya Kikwete (kushoto) akikagua gwaride rasmi na Rais George Bush wa marekani mud amfupi uliyopita jijini Dar es Salaam. hizi picha ni latest kabisa, kaeni mako wa kula kwa ma picha zaidi. Picha kutoka kwa http://haki-hakingowi.blogspot.com/


Air Force One

dege la Bush likitua

mguuuu sawa!

Rais George Bush wa Marekani na mai waifu wake Laura wakiwasili

Rais George Bush na mama wa kwanza wa marekani wakiteremka toka ndegeni

JK akimpa tafu mgeni wake wakati wa kukagua gwaride

ujio wa george w. bush

mh. Sofia Simba akimkaribisha bongo Condoleezza Rice

Rais Bush akisalimiana na waziri wa mabo ya ndani mh. Lawrence Masha

Rais Bush akionekana kusifia tenge alilokula mh. Margareth Sitta

Rais George Bush akisalimianaa na katibu mkuu wizara ya mambo ya ndani mh. Patrick Mombo na mbele ni katibu mkuu kiongozi mh. Philemon Luhanjo

JK na mgeni wake
Picha na http://issamichuzi.blogspot.com


Ujio wa Bush


Jamaa wa United States Secret Service na mbwa wake
wakicheki kama kuna noma

Waandishi wakiwa wamezungukwa na jamaa wakisuburi mgeni
Majamaa walikuwa hawaamini mtu


Makachero wa United State Secret Service wakivinjari
Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere


mizinga 21 inaapigwa kwa heshima ya George W. Bush
Picha na http://issamichuzi.blogspot.com



Rais Bush apokewa

na mamia wa wakazi

wa Dar es Salaam



*Usafi wa ziada wafanywa maeneo atakayotembelea

*Chadema wamtumia ujumbe amrejeshe Ballali

Na Waandishi Wetu


RAIS wa Marekani, George W Bush jana aliwasili nchini Tanzania katika ziara ya kitaifa itakayochukua siku nne.

Ujio wa Bush nchini unatokana na mwaliko wa Rais Jakaya Kikwete alioutoa mwaka jana akiwa nchini Marekani na una lengo la kukagua miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Marekani na mafanikio ya msaada katika kudhibiti maradhi ya ukimwi na malaria.

Bush aliwasili katika Uwanja wa Julius Nyerere saa 12:45 jioni akiambatana na mkewe, Laura; na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Condoleezza Rice na kupokelewa na mwenyeji wake Rais Kikwete.

Kabla ya ndege ya Rais Bush kuwasili uwanjani, ndege aina ya Boeing 747 Air Force Two namba 29000 iliwasili na maafisa wa Marekani zaidi ya 300.

Muda mfupi baadaye, ndege ya Rais huyo, Air Force One yenye namba 28000 na jina lake iliwasili. wakati inatua magari kama 10 ya makachero wa Marekani yaliifuata kwa kasi na kugeuza kisha kuegeshwa kwa pamoja.

Kupitia mlango wa nyuma kwanza waliteremka watu zaidi ya 100 kutoka katika ndege hiyo; na baadaye ndipo Rais Bush akatokea mlango wa mbele.

Uwanja huo wa ndege ulikuwa chini ya ulinzi mkali na katika maeneo yote ambayo Bush angefikia ulinzi ulikuwa ukiongozwa na makachero kutoka Marekani, na mataifa mengine mbalimbali walipo makachero wa nchi hiyo. Pia makachero wa Tanzania, baadhi wakitoka Zanzibar walifurika katika uwanja huo.

Baada ya kulakiwa na mwenyeji wake Rais Kikwete na mkewe, Salma Kikwete, Bush alipokea salamu za heshima kutoka kwa majeshi ya ulinzi na usalama kisha akapigiwa mizinga 21 na kukagua gwaride la majeshi ya Tanzania.

Yawezekana Rais Bush akawa kiongozi wa kwanza kupigiwa mizinga 21 na kupeperushiwa bendera baada ya saa 12 jioni kwani kwa kawaida shughuli hiyo hufanyika kabla ya muda huo.

Baada ya hapo alisalimiana na mawaziri waliokuwa wamevalia vitambulisho, Spika wa Bunge, Samuel Sitta, Jaji Mkuu, Augustino Ramadhan, Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho, Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo na viongozi wengine wachache.

Baada ya kumaliza kusalimiana, waliondoka na msafara wake wenye magari makubwa yaliyowashtua watu waliofurika nje ya uwanja huo kushuhudia mapokezi hayo.

Msafara huo ulitanguliwa na magari ya polisi na usalama wa taifa 10, mengine yaliyotoka Marekani. Rais Bush alipanda kwenye gari maalum aina ya Cadillac mojawapo kati ya mbili zilizokuwa katika msafara huo.

Mapema, maeneo ya katikati ya Jiji la Dar es Salaam yalikuwa na watu wachache, hali iliyoonyesha wazi kuwa baadhi ya wananchi wengi walikuwa na hofu kutokana na ulinzi mkali, matukio ya ugaidi na baadhi ya barabara kufungwa.

Hata hivyo, katika maeneo ambayo Rais Bush alipita kutokea uwanja wa ndege mbali na barabara kufungwa kwa ajili ya magari, watu kadhaa walijiotokeza kumlaki, lakini waliambulia kuona magari na giza lilikuwa limeanza kuingia.

Baadhi ya wananchi waliozungumza na gazeti hili walielezea kuwa, ni bora Bush awe anakuja mara kwa mara Tanzania kama usafi utaimarishwa kwa aina waliyoona jana.

Hospitali ya Amana iliyopo Ilala jijini hapa ilikuwa ikisafishwa tofauti na ilivyozoeleka na kulikuwa na ulinzi mkali kufuatia eneo hilo kuwa katika ratiba ya kutembelewa na Rais Bush kesho.

Baadhi ya wafanyakazi walikuwa wakipiga deki barabara za ndani ya hospitali, wodini, pamoja na kupanda nyasi kando kando ya barabara inayoingia hospitalini hapo.

Kulikuwa na ugawaji wa mashuka mapya kwa wagonjwa waliolazwa katika hospitali hiyo huku pia kukiwa na wafanyakazi wapya wasio Watanzania hasa katika maeneo ambayo yanaelezwa kuwa Bush atatembezwa. Maeneo hayo ni maabara, kitengo cha dawa na eneo la masuala ya ukimwi.

“Niko hapa toka Jumatatu nimekuja kumuuguza baba yangu lakini nimeanza kuona mabadiliko makubwa sana kuanzia Jumatano, ambapo tulipewa mashuka mapya; na kumekuwa na usafi mkubwa ambao umekuwa unafanywa hapa,” alisema John Andrew.

Katika hospitali hiyo kumekuwa na pilikapilika za hapa na pale ambayo imekuwa inafanywa na wafanyakazi hao kuhakikisha kwamba mazingira yanakuwa safi.

Kulikuwa na maduka machache yaliyofunguliwa katika mitaa ya Kariakoo na pilikapilika za watu ambazo huwa kubwa siku za mapumziko kama jana hazikuonekana kuwepo.

Katika hatua nyingine, Kitengo cha Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), jana kilimtaka Rais Bush kuisaidia Tanzania kumrejesha aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT) Daud Ballali waliyesema kuwa yuko Marekani kufuatia tuhuma za ubadhirifu wa fedha zilizogunduliwa katika Benki Kuu ya Tanzania aliyokuwa anaiongoza kabla ya uteuzi wake kutenguliwa.

Katika ujumbe huo, pia walimtaka Bush kusaidia uchunguzi kuhusu kampuni hewa ya kufua umeme maarufu kama Richmond Development Company LLC inayodaiwa ilikuwa na usajili nchini mwake.

Habari hii imeandikwa na Mkinga Mkinga, Editha Majura na Festo Polea kutoka gazeti la Mwananchi.

No comments: