Wednesday, March 26, 2008

Brick & Lace waahidi makubwa kesho


na Khadija Kalili tarehe 27.03.2008

WASANII mahiri wa kundi la Brick & Lace wanaotamba na miondoko ya R&B kutoka Jamaica, wameahidi shoo ya aina yake watakapotumbuiza kesho katika fainali za kumsaka nyota wa Bongo ‘Bongo Stars Search’ zitakazorindima kwenye Ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.

Wakizungumza na waandishi wa habari jana kwenye hoteli ya Movenpick, wasanii hao ambao wanatamba na wimbo wao unaofahamika kama, ‘Your Love is Wicked’, walisema wamekuja Tanzania kuwapa raha na si vinginevyo.

Wamewataka mashabiki wa muziki kufika kwa wingi ili kupata burudani ya uhakika, ambako wamewaandalia vitu vya uhakika.

Kundi hilo liliwasili jana jijini Dar es Salaam na kufikia Hoteli ya Movenpick ambako kesho litaungana na wasanii mbalimbali katika kupamba fainali hizo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Benchmark Productions, ambao ndiyo waratibu wa shindano hilo, Rita Paulsen alisema kwamba maandalizi ya fainali za shindano hilo yamekamilika, hivyo mashabiki wajitayarishe kumpata mrithi wa mshindi wa BSS wa mwaka jana, Jumanne Idd.

Rita alisema, mshindi katika fainali hizo, atapatikana kutokana na kupigiwa kura na mashabiki, hivyo mashabiki wawapigie kura washiriki ambao wanaona wanafaa kutwaa taji hilo.

“Mashabiki wana asilimia yao ya kumteua mshindi, kadhalika na majaji nao tuna nafasi yetu ya kutoa kura kwa washiriki pia, hivyo kila shabiki anapaswa kutambua kwamba ana wajibu wa kumchagua yule ambaye anaona kwamba anafaa kuwa mshindi wa BSS 2008,” alisema Rita.

Washiriki watano watakaochuana katika fainali hizo na namba zao kwenye mabano ni Ellynema Mbwambo (BSS 16), Misoji Nkwabi (BSS 11), Maangaza Nyange (BSS 05), Yohana Simon (BSS 14) na Rogers Lucas (03).


Brick & Lace kutua Dar es Salaam


na Khadija Kalili, tarehe 26.03.2008





Brick & Lace. Picha kutoka:
http://www.brickandlacemusic.com


Sikiliza "Love is Wicked"






WASANII mahiri wa kundi la Brick & Lace wanaotamba na miondoko ya R&B kutoka Jamaica, wanatarajiwa kuwasili nchini leo, mahusus kwa ajili ya kupamba fainali za shindano la kumsaka nyota bora wa bongo katika Bongo Stars Search, zitakazorindima Ijumaa, katika mbanda wa Blue Pear, Ubungo, Dar es Salaam.

Brick na Lace ambao wimbo wao unatamba katika kumbi mbalimbali za burudani unaofahamika kama ‘Your Love is Wicked’, watazungumza na waandishi wa habari, kwenye ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), mara baada ya kuwasili nchini.

Akizungumza jijini, jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Benchmark Productions, waratibu wa shindano hilo, Rita Paulsen, alisema kwamba maandalizi ya fainali za shindano hilo, yamekamilika, hivyo mashabiki wajitayarishe kumpata mrithi wa aliyekuwa mwasisi na mshindi wa BSS wa mwaka jana, Jumanne Iddi.

Rita alisema mshindi katika fainali hizo za Machi 28, atapatikana kutokana na kupigiwa kura na mashabiki, hivyo mashabiki wawapigie kura washiriki wanaoona wanafaa kutwaa taji hilo.

“Mashabiki wana asilimia yao ya kumteua mshindi, kadhalika na majaji nao tuna nafasi yetu ya kutoa kura kwa washiriki pia, hivyo kila shabiki anapaswa kutambua kwamba ana wajibu wa kumchagua yule anayeona kwamba anafaa kuwa mshindi wa BSS 2008,” alisema Rita.

Washiriki watano watakaochuana katika fainali hizo na namba zao kwenye mabano ni pamoja na Ellynema Mbwambo (BSS 16), Misoji Nkwabi (BSS 11), Maangaza Nyange (BSS 05), Yohana Simon (BSS 14) na Rogers Lucas.

Chanzo: Tanzania Daima

No comments: