Mhariri mkuu wa gazeti la Mwanahalisi Saidi Kubenea (kulia)akiwa na Bw. Ndimara Tegambwage wakitoka nje ya ukumbi wa idara ya Habari MAELEZO leo mchana jijini Dar es Salaam ambapo waliongea na waandishi wa habari juu ya vitisho ambavyo wamekuwa wakiendelea kuvipata tangu Kubenea alipotoka nchini India kutibiwa baada ya sakata la kumwagiwa tindikari.
Akizungumza na waandishi wa habari leo asubuhi, Kubenea amesema kuwa, Machi 5 siku ambayo alikuwa akitimiza siku 60 tangu ofisi yao ivamiwe mtu mmoja alimpigia simu katika simu yake ya mkononi na kumtaka asali sala yake ya mwisho. Hata hivyo amesema kuwa simu ya mtu haikuonesha namba(Private)"Sali sala yako ya mwisho"ameeleza Kubenea.
Mbali na simu hiyo Kubenea amesema kuwa siku tano nyuma kabla ya kupokewa simu hiyo alitumiwa ujumbe mfupi kwa njia ya simu ya mkononi 'sms'uliosheheni matusi ambayo hawezi kuyataja hadharani na akataja sehemu ya ujumbe huo kuwa ulikuwa ukisema:"Hivi wewe umekosa habari za kuandika magazetini eeh sasa basi kama umechoka kuishi tutakuondoa duniani kuanzia sasa,"ilieleza sehemu ya ujumbe huo.
Amesema vitisho hivyo sio vidogo kwa mtu yoyote yule na huu ni mwendelezo wa vitisho kwa miezi sita ambavyo ni pamoja na kugongwa na gari, kuchomewa gari,kusutwa,kutukanwa na kutishiwa kwa njia ya simu.
Kutoka: http://haki-hakingowi.blogspot.com
No comments:
Post a Comment