Thursday, March 27, 2008

Kikwete azindua shirika la

utangazaji Tanzania (TBC)



Raisi Jakaya Mrisho Kikwete,akisoma hotuba wakati wa uzinduzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) jana mchana jijini Dar-es-salaam.TBC imezinduliwa upya rasmi jana pamoja na nembo/logo mpya ya shirika hilo.Kuanzia sasa, iliyokuwa Televisheni ya Taifa (TVT) itaitwa TBC-One na iliyokuwa Radio (PRT) itaitwa TBC-FM na pia kutakuwepo na External Service itakayoitwa TBC International.

Wengine pichani (kulia kwa JK) ni First Lady,Mama Salma Kikwete na Tido Mhando ambaye ndio Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo.Kabla ya kurudi Tanzania kushika wadhifa huo mpya,Tido Mhando alikuwa Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza(BBC)




Nembo mpya ya Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC).Nembo ina kauli mbiu ya Ukweli na Uhakika. Ni matumaini yetu kwamba hivyo ndivyo itakavyokuwa na si vinginevyo.Picha zote na Ahmad Michuzi.

Habari toka Bongo Celebrity


No comments: