Saturday, March 29, 2008

Udaku wa Jumamosi


Na Mariam Mndeme.

Kauli ya mwanamuziki anayevuma hivi sasa nchini, Nakaaya Abraham Sumari, kuhusu sura na umbo lake vinawadatisha wanawake wenzake, imezua minong’ono kwamba huenda msanii huyo ni msagaji...

Msikilize Nakaaya na wimbo wake "MATATIZO"






Nakaaya kupitia kipindi cha Friday Night Live cha Luninga ya EATV, Ijumaa iliyopita alisema kuwa uzuri wake unawadatisha watu wa jinsia tofauti, hivyo hashangai wanawake wenzake kumtongoza.

Kabla ya kauli hiyo ya Nakaaya, mtazamaji mmoja mwanamke, alituma ujumbe wa simu ya mkononi (sms) na kusomwa na mtangazaji wa kipindi hicho, Denis Busulwa ‘Sebo’, akieleza jinsi anavyovutiwa na msanii huyo.


Msikilize Nakaaya na wimbo wake "Mr. Politician"





Kwa mujibu wa ujumbe huo wa maneno na jinsi ulivyosomwa na Sebo ni kwamba mtazamaji huyo wa kike, alikuwa akivutiwa na Nakaaya kimapenzi.

Mara baada ya kuiona sms hiyo, Sebo alimuuliza Nakaaya kuwa iweje awavutie mpaka wanawake wenzake?

Hata hivyo, msanii huyo alijibu kwamba yeye anawavutia watu wote, kauli ambayo ilitafsiriwa na baadhi ya watazamaji kuwa pengine anapenda ‘hako kamchezo’ ndiyo maana hakuchukia kutongozwa na mwanamke mwenzake.

“Huyu dada naye yumo nini katika mambo hayo, maana jibu lake linaonesha anaona poa tu kutongozwa na wanawake wenzake!” Alisema mtazamaji mmoja, katika baa moja iliyopo Sinza, jijini Dar es Salaam, huku mwandishi wetu akimsikia.

Katika kipindi hicho, Nakaaya alialikwa akiwa na mwenzake Jacqueline Ntuyabaliwe ‘K-Lyn’ pamoja na wanamuziki nguli wa R&B duniani, Wamarekani KCI & Jojo.

Wasanii hao wote, walikuwa wakizungumzia ‘shoo’ ya KCI & Jojo, iliyoandaliwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo ambapo Nakaaya na K-Lyin waliisindikiza katika Ukumbi wa Hoteli ya Movenpick jikjini Dar es Salaam Jumamosi iliyopita.

Aidha, siku moja baada ya kipindi hicho, habari tulizozipata kutoka kwa rafiki wa Nakaaya zilisema kuwa msanii huyo amekuwa akipigiwa simu na wakati mwingine kutumiwa ujumbe na idadi kubwa ya wanawake wakimtongoza.

Rafiki huyo alisema: “Wanawake wengi wamekuwa wakijieleza eti wanavutiwa na Nakaaya kwa sura yake halisi (natural), umbo, mtindo wake wa kukata nywele fupi na sauti yake.”

Nakaaya ambaye ni dada wa Miss Tanzania na Miss World Africa mwaka 2005-06, Nancy Abraham Sumari kwa sasa ‘anafunika’ katika anga ya burudani kupitia kibao chake cha Mr. Politician kilichobeba jina la albamu yake yenye jumla ya nyimbo 10.

Nyimbo hizo zinazopatikana katika albamu hiyo inayogombewa vilivyo sokoni ni Nervous Conditions, Mr. Politician, Matatizo, New day, Malaika, Iyeyo, Love me, Nyimbo za Uhuru, A town girl na I’m Free


1 comment:

Anonymous said...

I agree. Her second video Matatizo also shows she has a much better voice than people gave her credit for. you can buy her album on cdbaby.com/nakaaya