Na Mwandishi WetuWazungu kutoka nchi mbalimbali ulimwenguni wamebainika kudatishwa kimapenzi na mabinti wa Kitanzania kiasi cha kutumia fedha nyingi ili kuwanasa.....
Uchunguzi uliofanywa kwa muda mrefu na Amani ndani ya jiji la Dar es Salaam umebaini kuwa, baadhi ya wazungu hao hasa kutoka nchi za Uingereza, Uholanzi na Ujerumani waliopo nchini kikazi ama kitalii, wamekuwa wakipenda sana kuwa na uhusiano na ‘dada zetu’ kwa maelezo kwamba wanayajua mapenzi vilivyo.
Mmoja wa wazungu hao anayefahamika kwa jina la Livingstone raia wa Uingereza anayeishi Masaki jijini Dar es Salaam, aliliambia Amani kuwa wengi wao wanawapenda mademu wa kibongo kutokana na ukarimu wao na pia ustadi wao katika kuwaridhisha wanaume.
“Nawapenda kwa kuwa wanajua ‘how to love’ (Jinsi ya kupenda) na pia ‘they are so kind’ (Ni wakarimu sana),” alisema kijana huyo ambaye kwa sasa anafanya kazi na kampuni moja ya madini nchini.
Aidha, uchunguzi zaidi umebaini kuwa, baadhi ya wazungu hao wamefikia hatua ya kuwapangishia warembo hao nyumba za kifahari, kuwanunulia magari ya kutembelea na kuwahonga dola za Kimarekani kila wanapopatiwa huduma ya ngono.
Baadhi ya wasichana wa kitanzania wamekuwa wakiwapapatikia sana wazungu huku wengi wao wakiwa na ndoto za kuolewa nao ambapo baadhi yao wamefanikiwa na wengine kuachwa kwenye mataa.
Mmoja wa mamiss aliyewahi kushiriki mashindano ya Miss Tanzania miaka ya nyuma ambaye kwa sasa ni mwanamitindo alieleza kuwa, kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wazungu si kitu cha ajabu kwani nao pia ni watu.
“Sawa mimi bwana wangu ni mzungu na hajanioa ila malengo yetu ni kuoana, kwani wewe unaona hatari sana mimi kuwa na mtasha? Wenyewe wanadata na sisi na ndio maana wakitushobokea tunawakamua dola!” alisema mwanadada huyo mwenye figa halisi ya kibantu.
Amani linawaasa dada zetu kuwa makini na wazungu hao kwani baadhi yao wanaweza kuyayumbisha maisha yao kwa kuwachezea kisha kuwaacha solemba.
No comments:
Post a Comment