Thursday, April 03, 2008

Ajali ya ndege

Mwanza..


WATU wawili wamekufa katika ajali ya ndege ndogo iliyotokea leo jioni katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza. Kwa mujibu wa habari za kuaminika ni kwamba ajali hiyo ilitokea saa 10.15 jioni wakati ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria wanane iliyokuwa na abiria wawili, ilipogonga mlima na kuanguka. Chanzo cha habari kilisema, inasadikiwa kuwa watu hao wawili waliojulikana kwa jina mojamoja la Mathew na Chris ni raia wa Marekani na Australia ambao mmojawao alikuwa rubani na mwingine mwanafunzi.

“Inasadikiwa kuwa kilichotokea ni technical fault na hali ni mbaya hadi wakati huu tunazungumza bado ndege inaungua na mwili uko ndani,umeteketea kiasi cha kutotambulika,”. Kwa mujibu wa ofisa wa uwanjani hapo, mtu mmoja aliokolewa na alikufa akikimbizwa hospitalini. Hadi chanzo cha habari kinaondoka eneo hilo, bado vikosi vya uokoaji na zimamoto vilikuwa vikijitahidi kuzima moto huo.Habari hii na imeletwa kwenu na
Jacob Kambili kutoka Mwanza.


No comments: