Andrew Chenge:
Mtihani mwingine kwa JK
Mtihani mwingine kwa JK
Martin Malera
NILIPOANDIKA makala iliyobeba kichwa cha habari ‘Why Andrew Chenge?’ mara baada ya Rais Jakaya Kikwete kutangaza Baraza lake jipya la Mawaziri, baadhi ya wasomaji hawakunielewa, akiwamo Chenge mwenyewe, ambaye alinitumia ujumbe mfupi wa kejeli na matusi kwenye simu yangu ya kiganjani kuwa eti niache wivu wa kike na ni muulize aliyemteua (yaani Rais Jakaya Kikwete).
Niliandika makala hiyo kwa uchungu mkubwa huku nikimbebesha zigo la lawama Rais Kikwete kwa kuendelea kuwakumbatia wazee wanaopaswa kuwa wanacheza na vitukuu vyao saa hizi, kwani walishalitumikia taifa hili kabla hata ya kuzaliwa kwangu hadi sasa, lakini hawana jambo la maana walilolifanyia taifa zaidi ya kulifilisi kwa kujilimbikizia ukwasi wa kutisha.
Niliandika kupinga uteuzi wa Chenge kwani binafsi sikutarajia kumwona tena Andrew Chenge, Mwanasheria Mkuu wa zamani aliyehusika kutoa ushauri kwa serikali ya Benjamin Mkapa na hata kusaini mikataba mingi iliyotuachia maumivu makali kama ya IPTL, Net Group Solutions, ununuzi wa rada na dege mkweche la rais, na mingine bomu, ambayo sasa ni mzigo kwa taifa.
Nilihoji uhalali wa Chenge kubaki kwenye baraza, kwani ni mmoja wa watu 11 waliotajwa kwenye tuhuma za ufisadi na Dk. Willibrod Slaa. Hakika Chenge alichafuka, hajajisafisha na hawezi tena kuaminika kwa wapiga kura wake na anaowaongoza. Kulikuwa na ulazima gani kumrejesha?
Ninapo mzungumzia Chenge na tukio hili la ufisadi linalomwandama sasa, nakumbuka jambo moja lililokuwa gumzo kwa wananchi wa Bariadi Magharibi wakati wa uchaguzi mkuu wa jimbo hilo mwaka 2005, alipokuwa anachuana na Isaac Cheyo (UDP).
Gumzo hilo lilikuwa juu ya jumba la kisasa na la kifahari lililoshushwa na Chenge, miezi sita kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 ili kuhalalisha uasilia wake katika jimbo hilo.
Ukiachia jumba hilo, kampeni zake ambazo binafsi nilizishuhudia, zilikuwa kufuru na hakika ziliacha gumzo.
Jamani wa Tanzania, sina wivu wa kike kama anavyonikejeli Chenge, lakini taarifa za hivi karibuni kwamba nguli huyo anamiliki akaunti ya dola milioni moja, sawa na sh bilioni 1.2, tena ughaibuni katika Kisiwa cha Jersey, zinapaswa kumliza kila Mtanzania na kuamua kuchukua hatua mara moja ya kuhakikisha pesa hizo zinarejeshwa, endapo asipothibitisha uhalali wake.
Wananchi tunaweza kutumia nguvu ya umma iwapo serikali iliyopania kupambana na mafisadi, haitaki kufanya hivyo kama inavyomlinda Daudi Ballali na wengine waliohusika katika wizi wa fedha za EPA, na ambao wanajulikana, kwani wamo mitaani.
Shilingi bilioni moja si fedha nyingi kwa wafanyabiashara wakubwa, lakini kiasi hicho cha fedha kumilikiwa na Chenge ambaye si mfanyabiashara, bali ni mwanasiasa na mtaji wake ni nyadhifa anazoshika, kinatia shaka na hakika Chenge lazima atuthibitishie jinsi alivyozipata.
Watanzania upole umetuzidi kiasi cha kuwa mandondocha. Tumesikia mafisadi walivyoifilisi BoT, hakuna aliyeguswa, tena wengine wanaona kama vile fedha hizo haziwahusu, tumesikia mafisadi walivyogawana fedha za EPA, hakuna aliyeguswa zaidi ya kusoma taarifa hizo kwenye vyombo vya habari, tumesikia ufisadi wa Richmond na jinsi dude hilo linavyozidi kulikausha Shirika la Umeme nchini (TANESCO), lakini hakuna anayeguswa, sasa limeingia hili la Chenge. Niwaulize, Watanzania, mnataka mguswe wapi ndipo mshituke?
Tanzania si maskini kiasi hicho tunachokishuhudia, umaskini wetu umetokana na uroho wa wachache tuliowapa dhamana ya uongozi kujilimbikizia mali.
Hebu fikiria sh bilioni 1.2 zilizohodhiwa na Chenge, zingetosha kujengea madarasa mangapi mnayolazimishwa vijijini kujenga kwa kudhalilishwa?
Ufisadi wa fedha za EPA, Richmond, Net Group, BoT, Meremeta, IPTL, rada, dege mkweche la rais na mwingine kadha wa kadhaa, ungeweza kujenga hospitali na barabara ngapi nchini? Watanzania nani kawaroga kiasi cha kukosa uchungu na nchi yenu?
Kikwete, huu ni mtihani mwingine kwako. Mtimue Chenge haraka. Rais wangu unapaswa kutambua kuwa Chenge ni mmoja tu kati ya mawaziri na viongozi wengine wa serikali wanaomiliki mabilioni ya fedha katika akaunti zao nje ya nchi.
Serikali ikiamua kutafuta watu wenye fedha hizo haramu, wanaweza kuwapata, lakini tatizo ni kwamba bado rais wetu hajawa na dhamira hasa, ukiacha ile ya mdomoni ya kutaka kupambana na mafisadi nchini.
Wito: Watanzania, rais amezidiwa nguvu na mafisadi, lakini huu si wakati wa kukata tamaa. Tutambue kwamba tumepiga hatua. Kutambua kwamba tatizo ni dhamira za viongozi wetu kupambana na ufisadi, hii ni hatua kubwa.
Ujasiri wa waandishi kama wa Tanzania Daima, kupiga kelele na kuwanyoshea vidole viongozi mafisadi, ni hatua kubwa nyingine. Tusikate tamaa, bali tuendeleze mapambano na siku moja tutashangilia ushindi.
Wakati nawatia moyo hivyo, sitaki tubweteke na kufikiri kwamba baraza hili jipya, ukimwacha Chenge, sasa litatufikisha mahali. Hapana, na narudia, Hapana. Bado ni usiku, bado kuna kazi na tukijidanganya kuridhika na baraza hili jipya, tutaangukia kwenye shimo ambalo hatutatoka tena. Hawa ni wale wale, tuwape tu muda wa kumalizia kipindi kilichobaki cha miaka mitatu na mwaka 2010 tuiambie CCM sasa basi.
matintz@yahoo.com
0713260071
Kutoka gazeti la Tanzania Daima.

No comments:
Post a Comment