Monday, April 14, 2008


Rais Kikwete akatisha ziara ya Ulaya kushughulikia Zimbabwe


na mwandishi wetu

HALI tete ya kisiasa nchini Zimbabwe, imemlazimisha Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), Rais Jakaya Kikwete, akatishe ziara yake aliyoianza mwanzoni mwa wiki hii katika mabara ya Asia na Ulaya.

Rais Kikwete, katika ziara hiyo aliyoanza Jumatatu wiki hii na baadhi ya viongozi wa nchi za Afrika, kwa kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Kimahusiano baina ya India na Afrika, uliofanyika New Delhi kati ya Aprili 8 na 9, alitakiwa baada ya mkutano huo afanye ziara nyingine za kikazi katika nchi za China, Denmark na Uingereza, kabla ya kurejea nyumbani Aprili 19.Hata hivyo, kutokana na hali tete ya kisiasa katika Zimbabwe, ambayo imesababisha Tume ya Uchaguzi ya nchi hiyo kushindwa kutangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Machi 29, mwaka huu, Rais amelazimika kurejea nyumbani. Habari zilizopatikana jana kutoka ndani ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, zilisema Rais Kikwete amekatisha ziara hiyo, na badala yake amemwagiza Makamu wa Rais, Dk Ali Mohamed Shein, kumwakilisha katika shughuli ambazo zingefanywa na Rais katika miji ya Copenhagen, Denmark na London, Uingereza.

Kwa mujibu wa ratiba ya awali kuhusu ziara hiyo ya Rais, iliyotolewa na Ikulu siku moja kabla ya kuruka kwenda India, Rais Kikwete alipaswa kuwasili mjini Copenhagen, kati ya Jumatatu na Jumanne wiki ijayo.

Akiwa huko, Rais Kikwete angehudhuria mkutano wa kwanza wa Kamisheni iliyoundwa na Waziri Mkuu wa Denmark, Anders Rasmussen, inayolenga kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya vijana na ajira barani Afrika.

Kazi hiyo sasa atalazimika kuifanya Dk. Shein, kwa kuwa Rais Kikwete anatakiwa kuhudhuria mkutano wa leo wa Jumuiya ya Maendeleo kwa Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), ulioitishwa na Mwenyekiti wa jumuiya, Rais wa Zambia, Levy Mwanawasa, mjini Lusuka, ukiwa ni maalumu kwa ajili ya kuzungumzia hali ya kisiasa ilivyo nchini Zimbabwe.

Aidha, habari kutoka ndani ya wizara hiyo ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, zinasema baada ya ziara hiyo ya leo nchini Zambia.



No comments: