Friday, May 16, 2008

Inspekta Jenerali wa

Polisi, Saidi Mwema

Atoa Tamko Rasmi



Wadau Kama mlipata Taarifa leo kuwa wapemba walidai iwapo wenzao nane waliokamatwa na usalama wa Raia (jeshi la Polisi) na kuwekwa ndani kwa madai kuwa ni wahaini baada kupeleka malalamiko yao UNDP kwamba Pemba imetengwa kama wasingeachiliwa basi wapemba wote 10,000 wangejisalimisha vituo vya polisi.

Hali ambayo imepelekea Mkuu wa Usalama wa Raia, (Jeshi la Polisi)Inspekta Jeneral Said Mwema Pichani (kulia)Kuamuru watu hao waliokuwa ndani kwa siku kadhaa waachiwe huru na uchunguzi wa kesi yao utaenda taratibu kwa mujibu wa Sheria. Awali Jeshi la Polisi lilitoa tamko kwamba watuhumiwa hao hawaruhusiwi kutembelewa /ndugu zao kwakuwa kosa lao la Uhaini ni kubwa. Habari hii na Mdau Mpoki Bukuku jijini Dar es Salaam





2 comments:

Anonymous said...

HEHE JAKAYA POLE KAKA YANGU, YOTE HII VIONGOZI MPUNGA YALE YA TANGA SCHOOL.KAMA HAWA VIONGOZI WANGEOMBA KAZI WALIZONAZO HAYA YASINGETOKEA.HAWA MAKAMANDA WA POLISI WAMESOMA? NI WANASHERIA? AU WALIFANYA KUMLIDHISHA YULE ALIYEWAWEKA MADARAKANI?WATU WAOMBE KAZI JAMANI KUTEUWA HUKU KUTATULETEA MATATIZO.

Anonymous said...

Wakati mwingine wanafanya maamuzi bila ya kushauriana na ya jazba. Matokeo yake ndiyo kama hayo