Thursday, May 15, 2008



Intaneti kwa lugha ya

Kiswahili yakamilika



na Dennis Luambano


MRADI wa kubadilisha taarifa zinazopatikana kwa lugha ya Kingereza kwenye mitandao, kwenda katika lugha ya Kiswahili umemalizika.

Kauli hiyo imetolewa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Kituo cha Mtandao wa Taarifa Tanzania (tzNiC), Prof. Beda Mutagahywa, wakati wa maadhimisho ya wiki ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEKNOHAMA).

“Mradi ule tayari umeshamalizika na una mambo mengi tofauti na watu wanavyodhani kwa sababu hauishii kwenye system peke yake, watu wanatakiwa waweke material yenye information tofauti.

“Kwa hiyo kuna mambo ya spelling check na vitu kama hivyo na naweza kusema kama kuna vitu ambavyo vitakuwa vimebakia basi ni vidogo vidogo tu ambavyo haviwezi kufanya tuseme kwamba haujakamilika,” alisema Prof. Mutagahywa.

Aliwataka vijana na watu mbali mbali ambao ni watundu na wanaoweza kutumia vizuri ‘internet’ waweke taarifa nyingi kwa lugha ya Kiswahili ili watu wengi waweze kuzielewa.



Angalieni baadhi ya mifano ya
maneno ya TEKNOHAMA


Chanzo:

http://www.kilinux.udsm.ac.tz/kiblog/kiblog_
sw/sw_TZ_glossary_klnX_1.html


accelerator
kichapuzi


allow popup from this site
ruhusu udukizi kutoka tovuti hii


Alt (Alternate)
(Kbdl) Kibadala


anonymity
ufichojina


back button
kitufe rejeshi


background color
rangi usuli


backslash(e)s
mkwajunyuma


BBS (Bulletin Board Service)
HUM (Huduma za Ubao wa Matangazo)



blind carbon copy (bcc)
nakala fiche (bcc)


browser
Kivinjari


control panel
paneli dhibiti


country code
msimbo nchi


default search engine
injini-tafuti msingi


double-click
bofyabofya


download
pakua


drag and drop
kokota na dondosha


FAQ (Frequently Asked Questions)
MYM (Maswali Yaulizwayo Marakwamara)


freeware
programu dezo



FYI (For Your Information)
KTY (Kwa Taarifa Yako)


keyboard
baobonye


LAN (local area network)
LAN (mtandao kiambo)


multiple recipient
wapokezi anuwai


password
nywila


popup (n)
kidukizo (n)


screensaver
kilezi


sidebar
mwambaa pembe


spell-checker
kikagua tahajia


toolbar
mwambaa zana


URL (Uniform Resource Locator)
KISARA (Kioneshi Sanifu Rasilimali)


webmaster
mtawala tovuti


web page
gombo wavu


website
tovuti


word processor
kichakata matini




No comments: