Monday, May 26, 2008

Kuituhumu serikali bila

ushahidi si ustaarabu


Mhariri
Daily News
; Monday,May 26, 2008


KATIKA siku za karibuni kumekuwapo na maneno mengi hasa kutoka kwa wanasiasa, wakionyesha hisia zao kwamba kuna mkono wa mtu katika kifo cha aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu, nchini, Dk. Daudi Ballali.

Kauli zao za kushtusha si tu zimeelekezwa kwa serikali, bali kwa mfumo mzima unaotengeneza serikali hiyo na hivyo kuleta walakini katika akili za watu wengi wanaotafakari mambo wakiwa na akili timamu.

Kutokana na kauli hizo ambazo pia zimetoa hoja za kuundwa kwa tume kuchunguza mazingira ya kifo hicho kunaonyesha ni kiasi gani watu wanaweza kuamua kufuata uzushi na kuufanya kuwa ukweli.

Kutokana na mazingira mazima ya tukio hilo tungelipenda kuunga mkono tamko la serikali la kutaka mtu mwenye ushahidi wa kidaktari kuhusu kilichotokea autoe badala ya kuendelea kuipakaza matope serikali na kusambaza uvumi unaojenga chuki kwa wananchi.


Bofya na endelea kusoma......

No comments: