Nchi imetekwa na
genge la Mafia?
KWA lugha ya kigeni linaitwa “Mafia group,” yaani “Genge la uhalifu.”
Linaweza kuwa la ndani, la kimataifa au yote kwa kushirikiana katika nchi moja.
Katika nchi kama Italia, Columbia, Marekani na hata Urusi, genge hili lina nguvu sana, na serikali yoyote ikitaka kupambana nalo, inapaswa kujizatiti kikamilifu.
Huendesha serikali isiyo rasmi, lakini yenye nguvu kuliko hata serikali halali madarakani. Huendesha biashara kubwa kwa magendo ikiwamo pia ile inayoitwa biashara haramu ya fedha (money laundering) na biashara ya dawa za kulevya.
Lina vikosi vyake vya mauaji. Humuondoa yeyote anayeonekana kuwa kikwazo katika kutimiza malengo yake. Halijali cheo cha mtu, hata kama ni rais, waziri mkuu, jaji, mkuu wa jeshi la polisi au hata wakili “machachari” (mkali) anayepambana na mafisadi mbele ya sheria.
Mauji yanayofanywa na genge hili kwa walengwa wake yanaweza kuwa kwa njia ya kudhuru mwili au kudhuru kisiasa. Genge la Mafia linaweza kupenyeza watu wake katika taasisi nyeti za utawala wa nchi, ukiwamo utumishi wa umma, kuhakikisha kwamba serikali inatumikia uharamia zaidi kuliko kutumikia umma, na mipango ya nchi kulenga kunufaisha maharamia wa kimataifa na washirika wake nchini badala ya malengo ya kitaifa kwa ustawi wa wananchi.
Bofya hapa na endelea kusoma...
No comments:
Post a Comment