Ndugu zanguni
nifahamisheni…
Hivi huyu binti alipokamatwa alikuwa anaziuza waziwazi hizo picha mitaani? Hapana kutokana na taarifa za gazeti la Risasi Mchanganyiko....
Kama angekuwa anatembea nazo waziwazi hizo picha, ningeelewa lakini..!!??
Maskini binti wa watu kakutwa na picha 4 ambazo zilikuwa kwenye mfuko wake. Picha zake binafsi. Mimi kwa fikra zangu finyu nadhani hakufanyiwa haki kufungwa kwa mwaka mmoja kwa kukutwa na picha 4 zake mwenyewe binafsi. Watu ambao hawajui jela zilivyo...binti wa watu akitoka atakuwa keshaharibika zaidi....Jela Tanzania si mchezo...si mwanamke si mwanamme..mambo ya huko wanayajua walioko huko na ambao walikuwa huko....
Polisi mbona hawavifungi vibanda vinavyoonyesha picha na kanda za ngono vilivyozagaa jijini Dar es Salaam? Na vingi vinajulikana? Hebu jamani nielewesheni...haki iko wapi hapa? Kuna mantiki yoyote?
"Nimelazimika kutoa adhabu hii kali kwa kutambua kwamba taifa letu liko katika vita kali ya kupambana na ugonjwa hatari wa Ukimwi," alisema hakimu Kamwela.
Ebo...kwa kumfunga dada wa watu kwa kumkuta na picha 4 alizokuwa nazo kwenye pochi yake? Picha zake binafsi?
Kama ni hivyo basi, mbona biashara ya kale kuliko zote duniani (biashara ya umalaya) inaendela kila kukicha? Wauzaji na wateja wanadunda tu bila kukamatwa na kufungwa....haki iko wapi?
....Kabla ya kutoa hukumu hiyo, Mwendesha Mashitaka PC, Kingazi aliiomba mahakama hiyo itoe adhabu kali kwa mshitakiwa kwa kuwa tabia kama hiyo inakwenda kinyume na maadili ya Kitanzania.....
Hapa nimeaachwa mbali (sijui nikisema nimeachwa kwenye mataa nitaonekana mtu wa miaka ya 47..??!!) ..sijui nicheke ama nilie...mbona maadili mengine yanayoharibiwa na tena mabaya zaidi hayashughulikiwi?
Mbona haya magazeti ya udaku yalichapisha hizo picha hayajafungiwa?
wenu,
Jamaldeen T. Bin Mazar E. Shariff Ibn Zenjibari

Na Dunstan Shekidele, Morogoro.
Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Kamwela alisema kuwa, alimtia hatiani Violet kwa kutumia kifungu na. 176, sura ya 16 ambapo adhabu ya kosa la kupiga ama kumiliki picha za uchi ni kifungo cha miezi 12 jela.Mkazi wa mjini hapa Miss Violet James (25), amehukumiwa kwenda jela mwaka mmoja baada ya kukiri mahakamani kuwa alipiga picha za uchi kwa lengo la kumpelekea mchumba wake nyumbani kwao mkoani Mtwara....
Violet alihukumiwa kifungo hicho na Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo ya Mazimbu, Lucia Kamwela Mei 8, mwaka huu.
"Nimelazimika kutoa adhabu hii kali kwa kutambua kwamba taifa letu liko katika vita kali ya kupambana na ugonjwa hatari wa Ukimwi," alisema hakimu Kamwela.
Kabla ya kutoa hukumu hiyo, Mwendesha Mashitaka PC, Kingazi aliiomba mahakama hiyo itoe adhabu kali kwa mshitakiwa kwa kuwa tabia kama hiyo inakwenda kinyume na maadili ya Kitanzania.
Kufuatia hukumu hiyo, Violet alipandishwa kwenye Karandiga huku akimwaga chozi tayari kwa safari yake ya kwenda kuanza maisha mapya gerezani.
Violet alikamatwa Aprili 24, mwaka huu akiwa na picha 4 za utupu kwenye mkoba wake kufuatia polisi ‘kutonywa’ kuwa miss huyo anatembea na picha zake za utupu.
Mara baada ya kukamatwa, miss huyo alipekuliwa na kukutwa nazo ambapo alifikishwa kituo Kikuu cha Polisi na kufunguliwa jalada MOR/IR/2619/08 ambapo alifikishwa mahakamani kujibu shitaka.
Naye Mkuu wa Makosa ya Jinai mkoani Morogoro, Ahamed Zahoro Msangi alisema msako unaendela kwa watu wengine wenye tabia za kuwapiga, kupiga na kumiliki picha za utupu kwani ni kosa la jinai.
Hivi karibuni kumekuwa na matukio kadhaa ya watu kupiga picha chafu katika maeneo mbalimbali nchini ambapo Miss Ilala namba 3 mwaka 2005, Jacqueline (pichani mbele) akiwa na marafiki zake walirekodi mkanda wa video uliokuwa ukionesha vitendo vya ngono huku baadhi ya warembo wakivua nguo zote.
Hata hivyo, Jacqueline baadaye aliutolea maelezo mkanda huo kuwa ulikuwa ni wa ‘kicheni pati’ ya mrembo mwenzao aliyekuwa akifundwa kabla ya kufunga ndoa.
8 comments:
Jamaldeen,
heko mwana umenena....hyo dada hata mwakili wa kumtetea hakuwa hakuwa naye...labda angewekewa wakili maswali hayo uliouliza hakimu angeshindwa kuyajibu...ndivyo Tanzania ilivyo....
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alisema kweli:
"Binadamu wazima na fahamu zao, huishi kama wanyama wa mwituni, ambao uhai wa kila mmoja wao hutegemea ujanja wake wa porini, ukali wa meno yake na urefu wa makucha yake. Upebari ni unyama"
Mbona Miss Ilala na. 3 mwaka 2005 hajapelekwa wala kushtakiwa mahakamani na kanda waliyorekodi ya "kitchen party"?
Dada wa watu ana damu ya kunguni!
JAMALDEEN DOH! INAONYESHA UNAOGOPA SANA JELA ZA BONGO EEEH?! UNAAMBIWA GEREZA LA UKONGA KUNA SEHEMU INAITWA MTWARA. UKIPELEKWA HUKO JAMAA WANAKUSHANGILIA
"MWALI KAINGIA...."
MIBABE ITAPIGANA KUKUGOMBANIA NANI WA KUKUANZA....USISIKIE...
WAKATI NIKIWA JESHI LA KUJENGA TAIFA (JKT) KRUTA MMOJA WA KIKE ALIJONGO (ALITOROKA) TOKA KAMBINI AKAENDA KWAO NA KURUDI BAADA YA SIKU 21. ALIPORUDI AKAHUKUMIWA NA COURT MARTIAL (MAHAKAMA YA JESHI) KUFUNGWA WIKI TATU UKONGA (JESHINI ENZI HIZO UKITOROKA NA KURUDI BAADA YA SIKU 21 UNAHUKUMIWA KUFUNGWA URAIANI) HUYO DADA AKAFUNGWA WIKI TATU UKONGA, KURUDI ALIKUWA ANATUHADITHIA KUWA HATA KWA WANAWAKE USIPOKUWA MKAKAMAVU, WANAWAKE WENZAKO WATAKUTUMIA NA KUKUFANYA MKE WAO, UWAFULIE NGUO NA ... (UNAJUA TENA) MAMBO YA USAGAJI YAMEJAA KWENYE JELA ZETU...ALIKUWA ANAHADITHIA..
Ulivyoanza na "Ndugu zanguni nifahamisheni..."
Nimekumbuka MSONGO enzi zile na wimbo wao:
"Ndugu zanguni nifahamisheni ni..nimwokoe nani..wa kwanza mama, pili baba nimwokoe nani... mke wangu na wanangu wote wananitegemea...
Wadau mnaukumbuka wimbo huo?
Nilikuwa naamanisha MSONDO
Ukistaajabu ya Mussa utaona ya Firauni
Post a Comment