Thursday, June 05, 2008

Aliyefungwa miaka 11

aeleza adha za gerezani


Na Restuta James


Kijana yatima aliyekaa gerezani kwa miaka 11, Gregory Adrian, ameibuka na kusimulia mateso ya ukiukwaji wa haki za binadamu yanayotokea jela yakiwemo ya ulawiti na utumiaji wa mihadarati.

Amesema mengine hayafai kusimuliwa hadharani na kuwaomba viongozi wa serikali na wabunge, kwenda huko wakashuhudie.

Gregory ambaye alikuwa karani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kahama, alidai kuwa, alifungwa kwa kubambikiwa kesi ya kuomba rushwa na kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu baada ya kutokea mtafaruku baina yake na wafanyabiashara wa ng`ombe.

Anaeleza kuwa, mbali ya ulawiti na ukiukwaji wa haki za binadamu, wafungwa wamekuwa wakipewa adhabu nzito na zisizostahili kwa mtu yeyote duniani. ...

Bofya na endelea>>>>>

No comments: