
Kundi D
Hispania imeonyesha nia yake ya kuwa mabingwa wa Ulaya baada ya kuwafunga Sweden. Goli la kwanza
Ugiriki yavuliwa ubingwa
Urusi 1 = Ugiriki 0
Warusi wamewavua Ugiriki ubingwa na kuwatoa kwenye fainali za mataifa ya Ulaya. Antonis Nikopolidis golikipa wa Ugiriki alifanya kosa la kijinga, akanyang´anywa mpira na Sergej Semak akampa pasi Konstantin Zyrjanov aliyefunga goli la pekee na la ushindi kwenye dakika ya 32. Nafasi ya kwanza kwenye kundi hili imechukuliwa na Hispania ikiwa na pointi 6, huku Sweden na Urusi zikiwa na pointi 3 kila moja. Mechi ya mwisho kwenye kundi hili itakuwa baina ya Hispania na Ugiriki / Sweden na Urusi. Sweden au Urusi lazima mmoja wao ashinde. Zikitoka sare hakutakuwa na dakika za nyongeza, zitapigwa penalti baada ya dakika 90.
No comments:
Post a Comment