Monday, June 02, 2008

Mkutano wa Sullivan

waanza leo


Na Daniel Mjema, Arusha


HUKU Jiji la Arusha likiwa limegubikwa na pilikapilika nyingi, marais kutoka nchi saba za Afrika, wamethibitisha kushiriki mkutano wa nane wa kimataifa wa Taasisi ya Sullivan, unaoanza leo jijini hapa.

Marais hao ni Jakaya Kikwete wa Tanzania, Omar Hassan Ahmed

Al-Bashir wa Sudan, John Kufuor wa Ghana, Armando Emilio Gebuza wa Msumbiji na Mwai Kibaki wa Kenya.

Wengine ni Paul Kagame wa Rwanda na Mohamed Abdelazi wa Jamhuri ya Kiarabu ya Saharawi na Rais Mstaafu wa Nigeria, Olesegun Obasanjo.

Pia Makamu wa Rais wa Uganda, Profesa Gilbert Balibaseka, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Marekani, Dirk Kempthorne na Waziri wa Kazi wa Afrika Kusini, Thoko Didiza.

Ujumbe wa Rais Kibaki, ndio uliovunja rekodi kwa kuwa na maofisa 60, akifuatiwa na Rais wa Msumbiji ambao utakuwa na maofisa 39.


Bofya na endelea>>>>>



No comments: